METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, April 9, 2020

MBUNGE WA JIMBO LA ILEMELA DKT ANGELINE MABULA YUKO IMARA ANACHAPA KAZI

Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline S.L Mabula Leo ameendelea kushiriki vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vinavyoendelea Jijini Dodoma.

Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Ilemela inawaomba wananchi wa Jimbo hilo kupuuza taarifa zisizo za kweli zilizokuwa zimesambazwa  kuwa Mbunge wao anaumwa na ameshindwa kuendelea na vikao.

Aidha wahalifu waliosambaza taarifa hizo wametakiwa kuacha mara moja kueneza taarifa zisizo za kweli na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakae endelea kufanya hivyo, taarifa zote zinazohusu Mbunge  zitatolewa na Mbunge mwenyewe au ofisi yake kwa utaratibu rasmi uliopangwa na unaokubalika.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com