Waziri wa Nishati, Dkt. Medrad Kalemani, (
katikati) akitoa maelekezo kwa wakandarasi wanaotekeleza ujenzi wa kituo cha
kupoza na kusambaza umeme cha Mponvu mkoani Geita baada ya kuridhishwa na kasi
ya ujenzi wa kituo hicho alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa
kituo hicho.
Muonekano wa sehemu ya mitambo ya katika kituo
cha kupoza na kusambaza umeme cha Mponvu kinachotarajiwa kukamilika mwishoni
mwa Mwezi Mei, 2020.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani
(katikati) akikagua mashine zilizofungwa ndani ya jengo la kuendeshea mitambo
(Control room) katika Kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mponvu mkoani Geita
baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.
Muoneko wa jengo la kuendesha mitambo (Control
room) katika Kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mponvu mkoani Geita.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani( kushoto)
na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel (kulia) wakipita katika tope wakikagua
eneo la ujenzi wa kituo cha kuchenjua dhahabu cha Geita, huku kukiwa na mvua
kubwa.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani
(kushoto)akizungumza na baadhi ya Viongozi kijiji cha Buyagu,( hawapo picha
)ili wakawaeleze wananchi wao kulipia
gharama za umeme ili waunganishiwe huduma hiyo, baada ya kuwasha umeme katika
kijiji hicho. Uwepo wa virusi vya Corona nchini kumezuia mikusanyiko ya watu
kwa lengo la kujikinga na kuchukuwa tahadhari.katikati ni Mbunge wa Busanda,
Lolensia Bukwimba
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani(
katikati) na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya
Geita, Josephat Maganga( kushoto) wakiwa katika eneo linalojengwa jengo la
utawala la eneo la uwekezaji mkoani Geita.
Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani(
kushoto) akipata maelezo ya ufungaji wa Mashineumba( Transfoma) katika kituo
cha kuchenjua dhahabu cha Geita kutoka kwa Kaimu Meneja wa Shirika la Umeme
nchini( TANESCO) mkoani Geita, Charles Msangi(katikati).
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amesema
kuanzia Mwezi Juni mwaka huu, Mgodi wa kuchimba dhahabu wa Geita (GGM) utaanza
kutumia umeme wa Gridi ya Taifa kuendesha shughuli zake baada ya Kituo cha
kupoza na kusambaza umeme cha Mponvu mkoani Geita kukamilika mwishoni mwa Mwezi
Mei, 2020.
Aidha alisema ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa
kituo hicho ambacho awali kilipangwa kukamilika mwezi Juni lakini kutokana na
kasi ya ujenzi wake kitakamilika mwishoni mwa Mwezi Mei na kuanza kusambaza
umeme kwa wateja ikiwemo GGM.
Dkt. Kalemani alisema hayo, alipofanya ziara ya
kikazi Aprili 25, 2020, mkoani Geita ya kukagua ujenzi wa kituo cha kupoza na
kusambaza umeme cha Mponvu, Kituo cha kuchenjua dhahabu cha Geita na kuwasha
umeme katika Kijiji cha Buyagu na Zahanati ya Musasa.
“kituo hiki cha Mponvu kitakuwa mkombozi mkubwa
wa nishati ya umeme ya kutosha na kwa gharama nafuu kwa wakzi wa Mkoa wa Geita
na mikoa jirani,pia Mgodi wa GGM utajiendesha kwa faida zaidi na kuliongezea
mapato taifa kwa sababu wataacha kutumia majenereta kuzalisha umeme ambao ni wa
gharama kubwa sana ukilinganisha na umeme unaozalishwa hapa nchini” alisema Dkt.
Kalemani.
Dkt. Kalemani alifafanua kuwa, mgodi wa GGM
utatumia umeme wa gridi ya taifa kutoka kituo cha Mponvu ambacho kitapokea
umeme wa njia ya kusafirisha umeme wa Kilovolti 220 kutoka kituo cha Bulyanhulu
mkoani Shinyanga hadi mkoani Geita yenye urefu wa kilomita 55.
Vilevile alieleza kuwa tayari njia ya
kusafirisha umeme wa Kilovolti 33 utakaotumiwa na mgodi huo yenye urefu wa
Kilomita 6.5 kutoka katika kituo hicho hadi ndani ya mgodi huo imekamilika na
kinachosubiriwa sasa ni kuunganisha umeme punde kituo hicho kitakapokamilika.
Dkt. Kalemani pia aliwasha umeme katika Kijiji
cha Buyagu,ambacho ni moja ya vijiji vinavyopitiwa na njia ya kusafirisha umeme
wa Kilovolti 220 kutoka Bulyanhulu hadi Geita ikiwa ni ishara ya kukamilika kwa
njia hiyo kwa asilimia 80.
Katika kukagua maendeleo ya usambazaji umeme
vijijini, aliwasha umeme katika zahanati ya Musasa na kuwataka wananchi wa eneo
hilo kuendelea kulipia ili waunganishiwe umeme.
Hata hivyo aliliagiza Shirika la Umeme Nchini,
( TANESCO) kuharakisha ufungaji wa Mashineumba( Transfoma) katika kituo cha
kuchenjua dhahabu mkoani Geita ambacho kiko katika hatua za mwisho kukamilika.
Dkt. Kalemani alirejea kusema kuwa lengo la
serikali ni kuhakikisha kuwa wachimbaji wote nchini wanaendesha shughuli za
uchimbaji kwa kutumia nishati ya umeme unaozalishwa nchini kwa gharama nafuu.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert
Gabriel alisema kuwa kituo hicho kikikamilika kitakuwa uwezo wa kuchenjua
dhahabu inayotakiwa katika ubora wa kimataifa na kitawasaidia wachimbaji wadogo
kunufaika zaidi na shughuli zao za uchimbaji tofauti na ilivyo sasa.
Gabriel aliwaomba wawekezaji kwenda kuwekeza
zaidi katika mkoa huo wa Geita kwa kuwa kuna umeme mwingi wa kutosha na gharama
nafuu kuendesha shughuli mbalimbali vikiwemo viwanda.
Vilevile aliishukuru Wizara ya Nishati kwa
kuhakikisha kuwa mkoa huo unakuwa na umeme wa kutosha ili kuvutia wawekezaji
wengi, kuwaunganishia umeme wa bei nafuu wananchi wa mkoa huo pamoja na
kujengwa kwa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mponvu ambacho kitawezesha
migodi yote katika mkoa huo kutumia umeme, na kuugawa katika mikoa jirani.
0 comments:
Post a Comment