METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, April 9, 2020

DC KASESELA,POLISI CHUNGUZENI KIFO CHA MTOTO WA NYAWENGA

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kutumbukia chooni kwa mtoto aliyekuwa anaishi katika mtaa wa Kijiweni kata ya Mshindo.

Alisema kuwa amepokea kwa masikitiko kifo cha mtoto wa Zamda Nyawenga alifariki kutokana na kutumbikia chooni.

Kasesela alisema kuwa ameliagiza jeshi la polisi wilaya ya Iringa kuhakikisha wanafanya uchunguzi wa kutosha kubaini cha kifo cha mtoto huyo.

Aidha Kasesela alilipongeza jeshi la zimamoto kufika eneo la tukio kwa haraka na kuanza kuutoa mwili wa mtoto huyo aliyetumbukia chooni.

Mkuu wa wilaya huyo ametoa wito kwa wazazi,walezi na wananchi wote kuwalinda watoto wao ili kuepukana na vifo visivyo vya lazima.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com