Waziri wa Madini Doto Biteko Katikati akiongoza wajumbe wa wizara nne kwa ajili ya kumsaidia Reuben Mtitu maarufu Mzee Kisangani ambae ni Mjasiliamali kutoka wilayani Ludewa aliye azisha kiwanda cha kutengeneza zana za madini ya chuma.
Waziri wa Madini Doto Biteko mwenye suweta na wananchi mbalimbali wakimsikiliza Reuben Mtitu maarufu Mzee Kisangani alipomtembelea kwenye kiwanda chake cha kutengeneza zana mbalimbali
Timu ya wataalam 9 kutoka wizara ya
Madini, Wiziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, wizara ya
Viwanda na Biashara na Wiziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (OR- TAMISEMI) imeundwa ili kumsaidia Mjasiliamali wa miaka 60 kutoka mkoani
Njombe wilaya ya Ludewa, Reuben Mtitu maarufu Mzee Kisangani ili kutimiza ndoto
yake ya kuwa bilionea baada ya kubuni kiwanda kinachotengeneza zana
zinazotokana na madini ya chuma.
Kamati hiyo imeundwa leo tarehe Machi
30, 2020 na Mawaziri Wanne wa wizara ya Madini Doto Biteko, Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mussa Zungu, OR-TAMISEMI
Mwita Waitara na Naibu waziri ya Viwanda na Biashara Mhandisi, Stella Manyanya,
katika kikao kilichofanyika ukumbi wa mikutano wizara ya madini jijini Dodoma.
Wengine waliohudhuria ni kutoka
Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Mazingira (NEMC) na Wataalam kutoka wizara
ya Madini na Tume ya Madini.
Akifungua kikao hicho, Waziri Biteko
amewaeleza wajumbe hao, kuwa lengo ni kujadili namna ya kumsaidia Mzee
Kisangani kwenye kila hatua kutoka mahali alipo ili ikibidi awe bilionea.
Ameongeza kuwa, mzee Kisangani hajui kusoma wala kuandika lakini ameonyesha
kitu ambacho kama Serikali inahitaji kumsaidia kwa kila hatua anayohitaji.
Biteko amesema, alipokuwa ziarani
mkoani njombe kuanzia Machi 13-16, alitembelea kiwanda chake ambapo kwa namna
kilivyo, lakini kinatengeneza zana mbalimbali za chuma kama vile, Mapanga,
Fyekeo, Visu, Majembe huku akiwa amewaajiri watu 30, kutokana na uthubutu na juhudi
alizonazo. Waziri Biteko akiwa ziarani katika eneo hilo aliahidi kukutana
atakutana na Mawaziri wote wanao husiana na shughuli zake ili kujadili namna ya
kumsaidia.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mussa Zungu, akichangia namna ya
kumsaidia, amesema wizara yake kupitia (NEMC) itahitaji andiko (Bussines Plan)
na kwamba wataalam wa eneo hilo watasimama ipasavyo kusaidia Mzee Kisangani kufikia
ndoto yake. Wakati Zungu akihitaji andiko, Biteko amesema tayari Chuo Kikuu cha
Mzumbe walishajitolea kumuandikia andiko la biashara (Business Plan) ya kiwanda
chake. Naye Naibu Waziri wa OR-TAMISEMI
Mwita Waitara, amesema kila mkoa
ulipewa agizo la kuandaa maeneo ya uwekezaji hivyo Mkuu wa Mkoa mkoani humo
atatoa eneo maalum kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha Kisangani kwenye eneo
lililotengwa.
Kwa upande wake, Naibu wa Viwanda na
Biashara Mhandisi, Stella Manyanya amesema kumekuwa na changamoto nyingi za
kuwasaidia watu wenye ubunifu hususani kutokana na vipengele vilivyowekwa
kisheria suala ambalo huwakatisha tamaa. Amesema wizara yake kupitia NDC, SIDO
na TIRDO kila taasisi itatoa mtaalam kwa ajili ya kumsaidia mjasiliamali huyu
ili afikie malengo.
Mkurugenzi Mkuu wa NDC, Prof. Damian
Gabagambi amesema mara baada ya kusoma taarifa za ziara ya waziri wa Madini
kupitia vyombo vya habari alituma wataalam kwenda kiwandani hapo na kuona namna
gani ya kumsaidia ili kuzalisha chuma na kuongeza uwezo wa uzalishaji.
Waziri Biteko ambaye alikuwa
mwenyekiti wa kikao hicho, amesema kwakuwa tunataka kuona matokeo ya huyu Mzee
kutokana na nguvu za serikali ndipo iliamriwa kuundwa kwa kamati ya wataalam wa
aina mbalimbali ambao ni wizara/taasisi kwenye mabano, Wilfred Machumu (Tume ya
Madini), Issa Mtuwa (Wizara ya Madini), Abbas Mruma (GST), Prof. Silvester
Mpanduji (SIDO), Prof. Madundo Mtambo Mkumbukwa (TIRDO), Dr. Yohana Mtoni
(NDC), Anorld Mapinduzi (NEMC), Leo Mavuka (TAMISEMI), na Dr. Hellen (Chuo
Kikuu Mzumbe.
0 comments:
Post a Comment