METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, March 23, 2020

WASAFIRI WATAKAOPITA MPAKA WA TUNDUMA KUWEKWA KARANTINI SIKU 14

Eneo la Tunduma ambapo ni Mpaka wa Tanzania na Zambia ambapo wasafiri wanao toka Nchi zenye Ugonjwa wa Virusi vya Corona kupitia mpaka huo watawekwa Karantini kwa gharama zao kwa muda wa siku 14.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe George Kyando akinawa mikono kwa maji yenye dawa katika Mpaka wa Tanzania na Zambia eneo la Tunduma wakati Kamati ya Ulinzi na Usalama ilipokagua maandalizi ya kuwaweka karantini wasafiri wanao toka Nchi zenye Ugonjwa wa Virusi vya Corona.
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Songwe wakinawa mikono kwa maji yenye dawa katika Mpaka wa Tanzania na Zambia eneo la Tunduma wakati wakikagua maandalizi ya kuwaweka karantini wasafiri wanao toka Nchi zenye Ugonjwa wa Virusi vya Corona.
Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Songwe imeanza utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli la kuwataka wasafiri waliotoka katika nchi zilizo athirika Zaidi na maambukizi ya Virusi vya Corona kukaa karantini kwa muda wa siku 14 kwa gharama zao.
Jana Wajumbe wa Kamati hiyo wametembelea eneo la mpaka wa Tanzania na Zambia uliopo Tunduma Mkoani Songwe ili kutathmini utayari wa kuanza zoezi la kuwaweka eneo tengefu yaani karantini wasafiri hao kwani mpaka wa Tunduma una watumiaji wengi zaidi kutoka nchi mbalimbali.
Wajumbe hao wamekubaliana kuanza mara moja zoezi hilo mbapo wasafiri hao watajitenga kwa gharama zao na kwa muda wa siku 14, ambapo zoezi hilo limeanza kutekelezwa rasmi Machi 23, 2020 usiku huku maandalizi ya maeneo na mahitaji mengine kwaajili ya kuwatenga yakifanyika.
Pia wameweka mkakati wa kufanya kaguzi mbalimbali katika nyumba za kulala wageni ili kubaini endapo kuna wageni ambao wataingia nchini kutoka nchi ambazo zimeathirika Zaidi na Ugonjwa wa Virusi vya Corona  kwa kutumia njia zisizo halali na kisha kukwepa kukaa karantini huku ulinzi ukiimarishwa Zaidi katika eneo lote la Mpaka.
Aidha wamewasihi wananchi wote kuendelea kuchukua hatua za tahadhari ili kujikinga na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kunawa kwa maji na sabuni, kujiepusha na mikusanyiko isiyo ya lazima kwani kinga ni bora Zaidi kuliko Tiba.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com