Na Mathias Canal, WazoHuru Blog
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa amepiga marufuku uuzaji wa Ethanol nje ya nchi ili kuimarisha upatikanaji wa malighafi hiyo hapa nchini na kuviwezesha viwanda vya ndani kuzalisha kwa wingi vitakasa mikono.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Viwanda Prof Riziki S. Shemdoe imeeleza kuwa Waziri Bashungwa amesema kuwa Marufuku hiyo itasaidia kukabiliana na mahitaji makubwa ya bidhaa hiyo ndani ya nchi.
Aidha, Waziri Bashungwa amewataka wenye viwanda vinavyozalisha Ethanol kuongeza uzalishaji ili kuhakikisha Ethanol inapatikana kwa wepesi hasa kwa kipindi hiki ambacho nchi inapambana na virusi vya Corona (COVID-19)
Prof Shemdoe amesema kuwa Sambamba na hilo Mhe Bashungwa amebainisha zuio hilo kuanza kutekelezwa kuanzia tarehe 27 Machi, 2020.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment