METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, March 6, 2020

RAIS MAGUFULI ATOA BILLIONI 15 KUMALIZIA UJENZI HOSPITALI YA MWALIMU NYERERE MARA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu(kushoto) akijadiliana jambo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi na Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima wakati walipokutana mkoani Marawakati Mawaziri hao walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyopo mkoani Mara.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu(kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi na Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima wakati walipokutana mkoani Mara wakati Mawaziri hao walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyopo mkoani Mara.

Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima akielezea jambo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu(kushoto) na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi wakati Mawaziri hao walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyopo mkoani Mara.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa kiasi cha shillingi Billioni 15 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyojengwa kwa miaka 40 bila kumalizika.
Haya yamebainika wakati wa ziara ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi katika hospitali hiyo kujionea maendeleo ya ujenzi wake.
Akizungumza mara baada ya kutembelea Hospitali hiyo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa Hospitali hiyo itakuwa masaada mkubwa kwa wananchi wa mkoa wa Mara hasa kwa huduma za matibabu ya kibingwa.
"Kutakuwa hakuna haja ya kwenda Hospitali ya Kanda Bugando kupata matibabu ya kibingwa kwani tunataka huduma za kibingwa zitolewe hapa hapa"alisema
Kwa upande wake Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema kuwa Shirika la Nyumba na Chuo Kikuu cha Ardhi kimepewa kazi ya kusimamia ujenzi wa Hospitali hiyo hivyo ameagiza kazi kufanyika usiku na mchana ili limalizike kwa muda uliopangwa.
"Tumekubaliana tarehe 17 mwezi huu wa tatu wawe wamekamilisha Wing C ili huduma za Mama na mtoto zinanze kutolewa kwa muda husika" alisema
Kwa upande wake Mkuu Mkoa wa Mara Adam Malima amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa fedha kwa ajili ya kumalizia hospitali hiyo iliyokwama kwa muda wa miaka 40 mpaka sasa.
“Hospitali hii imechukua awamu tano za marais kumalizika na tunamshukuru Rais kwa kuchukulia kipaumbele katika hili” alisema
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com