METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, March 4, 2020

MSAFARA WA KIJINSIA WAMPA SHAVU KIJANA MJASIRIAMALI

Mwakilishi wa Katibu MkuuIdara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi. Imelda Kamugisha akizungumza na wananchi wa mkoa wa Shinyanga wakati wa mapokezi ya msafara wa kijinsia ulifika mkoani humo kwa lengo la kutoa elimu ya kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Wasanii Shetta na G nako wakitumbuiza katika Eneo la nuzo nane Mkoani Shinyanga wakati Msafara wa kijinsia unaolenga kutoa elimu ya mapambano dhidi ya vitendo vya kikatili uliposimama mkoani hapo.

Baadhi ya wasaidizi wa kisheria wakitoa msaada wa kisheria kwa  waanchi wa mkoa wa Shinyangawaliojitokeza kuupokea msafara wa kijinsia unaolenga kutoa elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya vitendo hivyo.

Timu ya Msafara wa kijinsia unaolenga kutoa elimu juu ya madhara ya ukatili wa kiji sia umefakiwa kumpa  ubalozi na kumjuwezeshakijana .. baiskeli itakayomsadia kujikwamua kuchumi na kuwa mfano kwa vijana na jamii katika mapambano dhidi ya vitendo vya kikatii mkoani Shinyanga.
Hayo yamefanyika  jana mkoani humo wakatiwa mapokezi ya  Msafara wa Kijinsia kutokomeza ukatili unaolenga kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya kufanya vitendo vya ukatili wa kijinsia kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yatakayofanyika Kitaifa Simiyu Machi 08, 2020.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jmaii, Afisa Maendeleo ya Jmaii Mkuu Bi. Imelda Kmaugisha amesema kuwa Mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa wanafunzi na watoto wadogo wa kike kupata mimba nakuopewa katika umri mdogo.
"Hapa Shinyana kuna vitendo sana vya watoto wa kike na wananfunzi kupewa mimba wakiwa bado wadogo na kuolewa pia hili sio swa naomba tulikemee kwa nguvu moja" alisema
Aidha amwataka vijana hasa waendesha baiskeli, bodaboda na bajaji kuwa mabalozi wazuri wa kutoa taarifa katka vyombo vya usalama mara waonapo vitendo hivyo vikitokea kwani watakuwa wameisadia jamii kuondokana na vitendo hivyo vinavyokatisha ndoto hasa za watoto wa kike nchini.
“Wanaofanya vitendo hivi ni watu wa karibu na familia zetu wanawapa mimba watoto wetu tunanyamaza kisa ndugu wengine wazazi na walezi wanaowaozesha watoto wakiwa wadogo hili sio sawa kabisa" alisema
Akitoa shukrani zake mara baada ya kupewa ubalozi na baiskeli kwa ajili ya biashara Martin Christopher Matiku amishauri jamii ya mkoa wa Shinyanga kuwa pia mabalozi wazuri wa kuhakikisha wanakemea vitendo vya ukatili wa kijisia katika maeneo yao ili kuweza kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha vitendo vya ukatili wa kijinsia vinatokomea.
“Naushukuru huu Msafara wa Twende Pamoja naahidi nitakuwa Balozi mzuri na nitasaidiz kutoa elimu juu ya adhara ya vitendo vya ukatili naamini itasaidia kuokoa watoto wa kikena kiume na wanawake katika madhara haya” aliseNaye Mtoa Huduma za Kisheria mkoa wa  Shinyanga Anna Kadaso Mtao amesema kuwa kesi nyingi zinazopokelewa katika madawati hayo ni za vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa vipigo unynyasaji wa wanawake katika mirathi na kesi za wanaume wakinyanyaswa pia zipo ingawa bado sio nyingi zinztolewa taarifa,
Msafara wa kijinsia kutokomeza ukatili wa kijinsia upo katika mzunguko ulioanzia mkoa wa Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa, Tabora na umefika mkoani Shinyanga  kuelekea Shinyanga na utapokelewa mkoani Simiyu kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com