Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe (Mb) akijibu maswali ya wabunge wakati wa Bunge la kumi na nane Jijini Dodoma tarehe 6 Februari 2020.
Sehemu ya mawaziri akiwemo Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb), Waziri wa TAMISEM Mhe Suleima Jaffo na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mhandisi Hamad Masauni wakifatilia kipindi cha maswali na majibu akijibu maswali ya wabunge wakati wa BUnge la kumi na nane Jijini Dodoma tarehe 6 Februari 2020.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe (Mb) akijibu maswali ya wabunge wakati wa BUnge la kumi na nane Jijini Dodoma tarehe 6 Februari 2020.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Wizara ya Kilimo ipo katika hatua za mwisho kupeleka Bungeni mapendekezo ya mabadiliko ya Sheria ya Maendeleo ya Ushirika yatakayoendana na mahitaji ya sasa ambayo yatahusisha mabadiliko ya mfumo na muundo wa uongozi ili kuendana na mahitaji ya teknolojia na kuleta ushindani wa kibiashara.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Hussein
Bashe (Mb) ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma tarehe 6 Februari 2020 wakati
akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Mbinga vijijini Mhe Martini Mtonda Msuha aliyetaka kufahamu serikali ina mpango gani wa kurekebisha
Sheria ya Vyama vya ushirika ili kuondoa mapungufu yaliyopo, hususani kwa
upande wa uanachama na kuipa serikali nguvu za kisheria juu ya Vyama vya
ushirika.
Bashe amesema kuwa Ilani ya
uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2015 – 2020 (Ibara ya 22 (g)(iv) na 86 (a)
inaelekeza “Kuifanyia mapitio Sera ya
Vyama vya Ushirika na kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Ushirika na
upatikanaji wa takwimu zitakazosaidia kuandaa mipango na kuleta mageuzi katika
Sekta ya Ushirika na kuimarisha uchumi wa Taifa na Kuviimarisha vyama vya
ushirika kuwa na uwezo wa kutafuta masoko ya mazao ya wakulima ya ndani na nje
kwa kuweka mfumo madhubuti wa ukusanyaji, uchambuzi na uenezaji wa taarifa za
masoko na kutoa elimu juu ya uongezaji thamani na biashara“
Amesema kuwa Ushirika ni dhana
ya hiari, lakini Serikali ni msimamizi
mkuu wa vyama vya ushirika pale ambapo viongozi wake au vyama vyenyewe havitekelezi
malengo yaliyokusudiwa na dhamira ya kuanzishwa kwa sekta ya ushirika.
Serikali inakiri vyama
vinakabiliwa na changamoto za kiutendaji, usimamizi, viongozi kutokuwa waadilifu
na mapungufu ya kimfumo ya uendeshaji wa vyama vya Ushirika hapa nchini.
Hata hivyo, Bashe amesema vipo
baadhi ya vyama vya ushirika ambavyo vinafanya vizuri. Mfano, Chama cha
Ushirika cha Chai Mkonge, Mafinga na Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU).
Kadhalika Mhe Bashe ameongeza
kuwa Ushirika ndicho chombo cha kuwaletea wananchi maendeleo ya kiuchumi kwa kuwaunganisha
wakulima ili kuwa na nguvu ya pamoja katika kutoa huduma za ugani, upatikanaji
wa pembejeo na kutafuta masoko ya mazao.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment