Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na
Teknolojia Mhe. William Tate Ole Nasha
akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma kuhusu mashindano
ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) mwaka 2020 yatakayofanyika kati ya Machi 16 hadi 20
mwaka huu Jijini Dodoma .
Mkurugenzi
mkuu wa Idara ya wateja wakubwa Benki ya CRDB Bw. Prosper Nambaya akisisitiza
kuhusu Benki hiyo kuendelea kushirikiana na Wizara ya Elimu , Sayansi na
Teknolojia katika mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia
na Ubunifu (MAKISATU) mwaka 2020
yatakayofanyika kati ya Machi 16 hadi 20 mwaka huuJijini Dodoma .
Akizungumza
leo Februari 5, 2020, Jijini Dodoma,
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. William Tate Ole Nasha amesema
kuwa lengo la MAKISATU ni kuibua, kutambua , kuendeleza Ubunifu na Ugunduzi
unaofanywa na Watanzania ili kuchochea maendeleo katika sekta mbalimbali.
“
Mashindano haya yanatoa fursa kwa wabunifu na wagunduzi wa teknolojia
mbalimbali kujitangaza na kutangaza bunifu zilizozalishwa ambapo kaulimbiu ya mwaka huu ni ” Sayansi,
Teknolojia na Ubunifu kwa Uchumi wa Viwanda”. alisisitiza Mhe Ole Nasha
Akizungumzia
walengwa wa mashindano hayo Ole Nasha amesema kuwa ni Shule za Msingi; Shule za
Sekondari; Vyuo vya Ufundi Stadi; Vyuo vya Ufundi wa Kati; Vyuo Vikuu, Taasisi
za Utafiti na Maendeleo pamoja na mfumo usio rasmi.
0 comments:
Post a Comment