Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhuhu bidhaa za kiwanda cha vifaa vya umeme cha Afriab Jijini Dar es Salaam kinachozalisha vifaa mbalimbali ikiwemo transfoma, katika mwendelezo wa Ziara ya kutembelea viwanda Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Vifaa vya Umeme vinavyozalishwa na kiwanda cha Africab kilichopo Jijini Dar es salaam, kiwanda hicho kinatengeneza vifaa mbalimbali zikiwemo transfoma na nyaya za umeme.
Moja ya Transfoma inayotengenezwa na Kiwanda cha Africab kilichopo Jijini Dar es salaam, ambapo Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa alitembelea na kutoa rai kwa watanzania kutumia bidhaa zitokanazo na viwanda vya ndani.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Riziki Shemdoe na wamiliki wa kiwanda kuzalisha vifaa vya Umeme cha Tropical kilichopo Dar es Salaam, Bw.Charles Mlawa na Aloyce Ngowi baada ya kutembelea kiwandani hapo leo Februari 19, 2020 katika Mwendelezo wa ziara ya kutembelea viwanda Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Riziki Shemdoe wakisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kiwanda cha Tropical kilichopo Dar es Salaam, Bw. Aloyce Ngowi walipotembelea kiwandani hapo leo Februari 19, 2020 katika Mwendelezo wa ziara ya kutembelea viwanda Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya mashine za kutengeneza vifaa vya umeme zilizopo katika kiwanda cha Tropical kilichopo Jijini Dar es Salaam kama zinavyoonekana kwenye picha kiwanda hicho kinatengeneza vifaa mbalimbali zikiwemo transfoma, nyaya za umeme na soketi za umeme.
Waziri wa Viwanda na
Biashara Mhe. Innocent
Bashungwa amewataka wadau wa Viwanda na Biashara kuendelea kuunga mkono Serikali
ya awamu ya tano kwa kuendelea kutoa ajira katika viwanda vidogo na vikubwa ili adha ya ukosefu wa ajira kwa vijana Nchini.
Ameyasema hayo leo Jumatano katika mwendelezo wa ziara
yake ya kutembelea Viwanda vilivyopo Jijini Dar es salaam na kutoa rai kwa kwa
watanzania kutumia bidhaa zinazotokana na viwanda vya ndani ili kuongeza ajira
kwa vijana
“Hongereni kwa kumuunga mkono Rais wetu Magufuli kwa kuwapa
ajira watanzania 150, ambao ni wahitimu wa vyuo mbalimbali hapa nchini, lakini hata wale walikuwa
nyumbani wamekaa bila kazi” alisema Mhe. Bashungwa
Katika Ziara hiyo Mhe. Bashungwa amewapongeza Bwana
Charles Mlawa na Aloyce Ngowi ambao ni wamiliki wazawa wa kiwanda cha Tropical
kilichopo Jijini Dar es Salaam kinachozalisha Vifaa vya Umeme (Soketi na Transfoma)
hapa Nchini kwa lengo la kuunga mkono Serikali kufikia Uchumi wa kati wenye
viwanda.
“Nyie ni wazalendo, ni mfano tosha kwa wawekezaji wazawa
kwa kufahamu umuhimu wa Serikali kufikia uchumi wa kati, transfoma na nyanya za
kupitishia umeme zote zenye ubora sasa zinatengenezwa Tanzania tena mwenge, Dar
es Salaam, na sio tena kuagiza kutoka nje ya Nchi” alisema Mhe. Bashungwa
aidha Mhe. Bashungwa alitoa rai kwa wananchi na wadau
wa sekta ya Viwanda na Biashara kuendelea kuunga mkono kwa kununua bidhaa za ndani zinazo tengenezwa na
wawekezaji wazawa na wazalendo.
“Niwaombe watanzania kuendelea kuipa kipaumbele neno ‘MADE IN TANZANIA’ utajisikiaje umeenda Nchi
za watu ukakuta chombo unachotumia kimewekwa nembo ya Tanzania, hakika ni
fahari sana” alisema Mhe. Bashungwa
Naye Mkurugunzi Mkuu wa kiwanda cha Tropical, Ndugu
Charles Mlawa ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuwaunga mkono na
kuwajali katika kuhakikisha sera na lengo la kufikia uchumi wa kati Nchini ifikapo
2025, kwani mpaka sasa kiwanda hicho kinapata umeme wa uhakika kutoka Tanesco.
“Nampongeza sana Rais Magufuli kwa kuendelea kutuunga
mkono sisi wawekezaji wa ndani, kwetu sisi ni fahari na tutaendelea kuiunga
mkono Serikali yetu” alisema Bwan. Mlawa
Waziri Bashungwa katika ziara yake, pia alitembelea kiwanda
cha AFRICAB kilichopo Kurasini Jijini Dar es Salaam kinacho jihusisha na
utenegezaji wa vifaa vya umeme vya majumbani, kinachomilikiwa na Wageni kutoka
India.
0 comments:
Post a Comment