Meneja Masoko na Huduma kwa Wateja wa NHIF
Bw. Hipoliti Lello akitoa mada kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Arusha kuhusu
mpango wa Vifurushi vya Bima ya Afya vilivyozinduliwa hivi karibuni.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw.
Christopher Mapunda akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa Habari Mkoani
Arusha,baada ya kuwapa elimu kuhusu mpango wa vifurushi vya Bima ya Afya.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw.
Christopher Mapunda akiongea na waandishi wa habari kuhusu mpango wa Vifurushi
vya Bima ya Afya ambapo aliwaeleza kuwa mpango huu utajumuisha kundi mkubwa la
watanzania ambao wapo nje ya mfumo wa Bima ya Afya.
Meneja wa NHIF Mkoa wa Arusha Bw. Isaya
Shekifu akiongea na waandishi wa habari Mkoa wa Arusha ambapo aliwasihi kuwa
mabalozi wazuri wa mpango huu wa vifurushi vya Bima ya Afya.
Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha
wakifuatilia mada zilizowasishwa na NHIF kuhusu mpango wa vifurushi vya Bima ya
Afya.
Mfuko wa Taifa wa bima ya leo umekutana na waandishi wa habari
mkoani Arusha kwa lengo la kuwaelimisha kuhusiana na vifurushi vipya vya bima
ya afya.
Akiongea wakati wa Mkutano huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw.
Christopher Mapunda amesema kuwa mpango huo
una lengo la kuhakikisha idadi kubwa ya watanzania wanakuwa na Bima ya
Afya ili kuwa na uhakika wa matibabu.
“Uanzishaji wa mango huu wa Vifurushi vya Bima ya afya ni fursa
kwa wananchi kujiunga na bima ya afya kuanzia kiwango cha 192,000 na
kuwawezesha kupata huduma ya uhakika wa bima ya afya.
Aidha, Bw. Mapunda alisema kuwa NHIF imeendelea kutoa elimu kwa
umma wa watanzania kuona umuhimu wa kuwa na Bima ya Afya kwa ajili ya matibabu
ya uhakika.
Akiongea kwa niaba ya Waandishi waliohudhuria Mkutano huo Mwenyekit
wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha Claud Gwandu alisema kuwa kwa
jinsi hali ilivyo sasa ni muhimu kwa kila mwananchi kujiunga na mpango huu
wenye nia ya kuwasaidia wananchi wengi zaidi.
“Hatukuwa tunaelewa namna vifurushi hivi vinavyofanya kazi, ila
baada ya elimu hii nimeona ndio suluhisho, watanzania waone umuhimu wa
kujiunga, kwasasa gharama za matibabu kwa sasa ni kubwa sana ila kwa vifurushi
hivi kwa mfano 192,000 inakuwezesha kupata matibabu kwa mwaka mzima”-Alisema
Bw. Gwandu
Naye Meneja wa NHIF Mkoa wa Arusha Bw. Isaya Shekifu amewashukuru waandishi
waliohuria kikao hicho na amewasihi kuwa
mabalozi wazuri wa vifurushi vipya vya bima ya afya.
0 comments:
Post a Comment