Mtakwimu Mkuu,
Dkt.Albina Chuwa akiwa katika picha ya Pamoja na Maafisa kutoka Ofisi ya Taifa
ya Takwimu mara baada ya kufua Warsha ya siku mbili Jijini Dar es Salaam leo
Januari 13, 2020.
Mtalaam
Mwandamizi wa Takwimu kutoka Ofisi ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa,Yannis
Derbali akieleza jambo kwa Mtakwimu Mkuu na maafisa kutoka Ofisi ya Taifa ya
Takwimu mara baada ya kufua Warsha ya siku mbili Jijini Dar es Salaam leo
Januari 13, 2020.
Ofisi ya Taifa ya
Takwimu kwa kushirikiana na Ofisi ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa imeendesha
Warsha ya Siku mbili kwa wataalamu wa Takwimu nchini kutoka, ili kuwezesha kuwa
na utaalam na ufanisi mkubwa katika kukusanya takwimu hasa kwenye kipingele za
matumizi bora ya Teknolojia mpya.
Akizungumza Jijini Dar
es Salaam Mtakwimu Mkuu, Dkt. Albina Chuwa amesema lengo la Warsha hiyo ni
kuwaandaa vijana kuendena na teknolojia ya sasa katika ukusanyaji takwimu,
kwani warsha inahusisha mafunzo ya rasimu
mpya ya methodolojia ya kupima kiashiria namba 17.14.1 cha Malengo ya Maendeleo
endelevu cha 2030(SDGs) kilichoandaliwa na Ofisi ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa.
“Ofisi ya Mazingira ya
Omoja wa Mataifa imefanya kazi kubwa kuandaa rasimu ya methodolojia ya kupima
kiashiria namba 17.14.1 cha malengo ya maendeleo endelevu, kwa hiyo kufanyika
kwa warsha hii kutasaidia vijana wetu kutoka na kitu kilichobora
kitakachosaidia kukusanya na kupata takwimu zilizobora na kitasaidia kuimarisha
mifumo ya kitakwimu nchini”, alisema Dkt. Albina Chuwa.
Dkt. Chuwa alisema
kuwa tangu mwaka 2015, Tanzania imepiga hatua kubwa katika kutekeleza Malengo
ya Maendeleo endelevu ya 2030, ikiwemo kufanya mikutano ya kutoa uelewa kuhusu
SDGs na kufanya kongamano la kujenga uwezo kwa mamlaka zote za Serikali za
Mitaa kuhusu SDGs na namna bora ya Kutekeleza.
Aidha Ofisi ya Taifa
ya Takwimu imeongeza ubunifu katika kuimarisha ushirikiano ambao unajumuisha
kwa karibu wadau katika kuboresha ikolojia ya takwimu nchini kwa ajili ya
kusaidia ugatuaji wa SDGs katika ngazi za kitaifa juhudi hizi zinalenga kujenga
msingi madhubuti wa upatikanaji wa Takwimu kwa ajili ya kusaidia upangaji na
ufuatiliaji mipango ya maendeleo yakitaifa na kimataifa.
Warsha hiyo ya siku
mbili kwa wataalamu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu inalenga kuimarisha uelewa
na teknolojia kwenye ukusanyaji takwimu ili kuweza kuendana Malengo ya
Maendeleo Endelevu ya Mwaka 2030.
Aliongeza kuwa Ofisi
ya Taifa ya Takwimu, inashirikiana na asasi mbalimbali za kiraia ili kuwezesha
kuwepo kwa uimara wa takwimu kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo kwenye
masuala ya elimu, Uchumi, Afya, kilimo na sekta zingine za maendeleo nchini.
“Ofisi ya Taifa ya Takwimu
inafanya kazi na Ofisi ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa katika kufanya
majaribio yay a rasmu ya methodolojia ya kupima kiashiria namba 17.14.1 cha
SDGs 2030 ambacho kinafuatilia Idadi ya nchi zenye mifumo ya kuimarisha
Mahusiano ya kisera kwa ajili ya mpango wa maendeleo endelevu kwa hiyo Warsha
hii itakuwa na manufaa makubwa kwa NBS”, alisema Dkt. Chuwa.
0 comments:
Post a Comment