METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, December 9, 2019

RAIS MAGUFULI ATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 5,533 MIAKA 58 YA UHURU



Katika kusherekea maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika (Tanzania Bara) Rais Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli ametoa msamaha wa wafungwa 5,533.

Akizungumza na Watanzania waliofurika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambako sherehe hizo zimefanyika kitaifa kwa mara ya kwanza kufanyika kanda ya ziwa Rais Magufuli  ameagiza wafungwa hao waanze kuachiwa kuanzia kesho.

“Nilitembelea magereza nikashuhudia kuna mlundikano wa wafungwa, mpaka leo kuna wafungwa 17,547 na mahabusu 18,256… Leo natangaza kuwasamehe wafungwa 5,533.  Hii ni mara ya kwanza kwa msamaha mkubwa kama huu kutokea, najua watu watashangaa lakini nimietumia siku hii ya uhuru kusamehe, sifurahi kuongoza nchi yenye watu wengi magerezani,” alisema na kuongeza:

“Msamaha huu utawahusisha wafungwa waliofungwa kati ya kipindi cha siku moja hadi mwaka mmoja, na waliofungwa miaka mingi wakiwa wamebakiza muda mfupi kumaliza vifungo vyao.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com