Katibu tawala wa mkoa wa Iringa Happiness Seneda akiongea na wadau wa elimu mkoani Iringa wakati tathimini na utangazwaji wa matokeo ya darasa la saba
Baadhi ya wadau wa elimu walioshiriki kikao hicho
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Katibu tawala wa mkoa wa Iringa
Happiness Seneda amewataka wananchi kuwa walinzi wa watoto wa kike ili kumaliza
tatizo la mimba za utotoni ambazo zimekuwa zinakatisha ndoto za watoto.
Kauli hiyo ameitoa wakati
akitangaza matokeo ya darasa la saba ya mkoani katika msimu wa mwaka huu wa
2019, Seneda amesemakuwa
kila wananchi anapaswa kuwa mlinzi wa kila mtoto ili afanikiwe kutimiza ndoto
zao.
Seneda alisema kuwa zambi ya
kuwapa mimba watoto wa kike haiwezi kuisha kwa kuwa ukifanya hivyo basi hata
mtoto wako atakuja kufanyiwa hivyo kwa kuwa malipo yapo hapa hapa duniani.
“Watoto wengi wanakatishwa
ndoto zo licha ya kuwa wengi wamekuwa wanaakili ambazo zingekuwa msaada kwa
maendeleo yake binafsi na taifa kwa ujumla hivyo wazazi na walezi wanawajibu wa
kuwafundisha tabia nzuri ili nao wajirindi na mimba za utotoni” alisema Seneda
Nao baadhi ya wadau
waliohudhuria kikao hicho wamesema kuwa kuna haja ya kubaridishwa kwa sheria
hiyo ili kuwabana wanaume wanaofanya vitendo hivyo kwa watoto wa kike.
0 comments:
Post a Comment