Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitupa udongo kwenye kaburi la kaka yake, Mzee Bakari Majaliwa katika mazishi yaliyofanyika kwenye kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika sala ya kumwombea marehemu kaka yake, Mzee Bakari Majaliwa iliyofanyika nyumbani kwa marehemu katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Simon Siro katika mazishi ya kaka yake Waziri Mkuu, Mzee, Bakari Majaliwa yaliyofanyika katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa
Taifa, Diwani Athumani katika mazishi ya kaka yake Waziri Mkuu, Mzee,
Bakari Majaliwa yaliyofanyika katika kijiji cha Nandagala wilayani
Ruangwa, Novemba 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na baadhi ya viongozi walioshiriki katika mazishi ya marehemu kaka yake, Mzee Bakari Majaliwa yaliyofanyika katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa , Novemba 6, 2019. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde, Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Simon Siro, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Venance Mabeyo na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Diwani Athumani. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali, Venance Mabeyo (kushoto), Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Simon Siro (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Diwani Athumani (kulia) baada ya wote kushiriki katika mazishi ya kaka yake Waziri Mkuu, Mzee, Bakari Majaliwa yaliyofanyika katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo katika mazishi ya kaka yake Waziri Mkuu, Mzee Bakari Majaliwa yaliyofanyika katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019. Wa pili kulia ni Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Simon Siro.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishirika katika sala ya kumwombea marehemu kaka yake, Mzee Bakari Majaliwa iliyofanyika katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
......................
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amewashukuru watu wote waliojitokeza katika mazishi ya kaka yake Mzee
Bakari Majaliwa (78), aliyefariki juzi (Jumatatu, Novemba 04, 2019)
nyumbani kwake katika kijiji cha Chimbila ‘B’wilayani Ruangwa, Lindi.
Ametoa shukrani hizo leo
(Jumatano, Novemba 06, 2019) wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika
kijijini Nandagala wilayani Ruangwa na amesema kwamba hayo ni mapenzi ya
Mwenyezi Mungu na kila mtu atapita kwenye njia hiyo.
“Tulikuwa 12 na sasa tumebaki
watano, wanaume wawili na wanawake watatu. Msiba huu kwetu ni mkubwa
umepunguza idadi ya watoto wa Mzee Majaliwa lakini hatuna namna ni
mapenzi ya Mwenyezi Mungu, wajibu wetu ni kuendelea kumuombea.
Nawashukuru wote mlioacha shughuli zenu na kutukimbilia, familia
imethamini sana ujio wenu jambao hili limetokea ghafla.”
Waziri Mkuu pia amemshukuru
Rais Dkt. John Magufuli kwa salamu za pole alizozitoa. “Jambo hili pia
limemgusa Mheshimiwa Rais wetu ambaye ametutaka tuwe watulivu katika
kipindi hiki kigumu na kwamba kila mmoja kwa dhehebu lake aendelee
kumuombea marehemu ili Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema.”
Amesema alipata taarifa za
msiba huo wakati akijiandaa kwenda wilayani Ruangwa kwa ajili ya
kushiriki mazishi yamwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa zamani wa CCM wa
Wilaya ya Ruangwa, Bw. Kaspar Selemani Mmuya.
Kwa upande wake, Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Generali, Venance Mabeyo akitoa salamu za
pole kwa niaba ya Maafisa na Askari wa Vyombo vyote vya Ulinzi na
Usalama amesema anajua uzito wa msiba pamoja na majonzi waliyonayo kwa
kuondokewa na mpendwa wao na kwamba wamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwa
ndiye anayetoa na anayetwaa. “Hakuna namna ya kurekebisha maamuzi ya
Mwenyezi Mungu, tuendelee kumsindikiza kaka yetu kwa sala Mwenyezi Mungu
ampokee kwa amani.”
Naye, Mwakilishi wa Mufti na
Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Othman Kaporo amesema amewataka wananchi
wajiandae na kifo kwa kufanya ibada. “Ni kawaida kwa binadamu kujisahau
lakini Mwenyezi Mungu ametuwekea vitu vya kutukumbusha juu ya uwepo
wake ikiwemo kifo, hivyo tuyatekeleze yale yalikuwa ya wajibu
kuyatekeleza.”
0 comments:
Post a Comment