Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya
pamoja na Wawezeshaji wa seina hiyo eneo la Mtumba katika Mji wa
Serikali leo jijini Dodoma mara baada ya kumaliza mafunzo ya kuwajengea
uwezo wajumbe hao juu ya Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2011 na
marekebisho yake ya mwaka 2016 pamoja na kanuni zake za mwaka 2013 ili
wawe na usimamizi sahihi wa mikataba yenye kuleta tija na thamani bora
ya fedha za Serikali.
(Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma)
……………………
Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma
Wataalamu wa Udhibiti wa Ununuzi
wa Umma (PPRA) wamesitiza Taasisi za Nunuzi kuandaa vizuri mpango wa
ununuzi na kusimamia utekelezaji wake ili mahitaji husika yaweze
kununuliwa na kupatikana kwa wakati.
Akizungumza na wajumbe wa Bodi ya
Zabuni ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo eneo la Mtumba
katika Mji wa Serikali jijini Dodoma, Mwezeshaji wa mafunzo ambaye pia
ni Afisa Ununuzi wa Umma kutoka (PPRA) Frank Yesaya amesema nia ya
mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wajumbe hao juu ya Sheria ya Ununuzi wa
Umma ya mwaka 2011 na marekebisho yake ya mwaka 2016 pamoja na kanuni
zake ili wawe na usimamizi sahihi wa mikataba yenye kuleta tija na
thamani bora ya fedha za Serikali.
Frank ameongeza kuwa ni muhimu
uwepo ushirikiano kati ya vyombo vinavyohusika na kufanya maamuzi na
kutekeleza shughuli mbalimbali katika mchakato wa ununuzi wa umma.
Vyombo hivyo ni pamoja na mamlaka
ya kuidhinisha bajeti, bodi ya zabuni, kitengo cha ununuzi, idara
tumizi, Kamati ya tathmini ya zabuni, timu ya majadiliano pamoja na
kamati ya ukaguzi.
“Ni muhimu kushirikiana, kila
mmoja atimize wajibu na majukumu yake bila kuingiliana hatua
inayopelekea mchakato wa ununuzi kuwa wa tijakatika ofisi husika.”
alisema Frank.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Idara ya Ununuzi na Ugavi Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Bi Cecilia Kasonga amesema mafunzo yanasaidia kuwaimarisha katika
kutekeleza majukumu yao ambapo ni vema mafunzo yatolewe mara kwa mara
ili kurahisisha kazi na kuwapa fursa wajumbe wa bodi kujua taratibu za
ununuzi wa umma hatua itakayosaidia kutoa maamuzi sahihi.
0 comments:
Post a Comment