Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea wakati
wa kutoa majumuisho yake katika semina ya wabunge wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Mpango wa Taifa wa
Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWA)
iliyomalizika leo Jijijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Bw. Peter Serukamba wakati wa
kutoa majumuisho yake katika semina ya wabunge wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Mpango wa Taifa wa
Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWA)
iliyomalizika leo Jijijini Dodoma.
Baadhi ya wabunge wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakifuatilia jambo
kuhusu Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia dhidi ya
Wanawake na Watoto (MTAKUWA) iliyomalizika leo Jijijini Dodoma.
……………….
Anthony Ishengoma -Dodoma
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema Sekta ya
Afya Nchini inachangia vitendo vya ukatili wa kijinsia hapa Nchini kwa
baadhi ya watoa huduma ya Afya kushiriki kuficha ushaidi kwa njia ya
rushwa.
Dkt. Ndugulile amesema hayo leo
Jijini Dodoma wakati wa kutoa majumuisho yake katika semina ya wabunge
kuhusu Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia dhidi ya
Wanawake na Watoto (MTAKUWA) iliyomalizika leo Jijijini Dodoma ili
kujenga uelewa kwa kamati ya Bunge kuhusu mpango huo.
Dkt. Ndugulile amesema watoa
huduma ya Afya wanawajibu wanapopata zile kesi zinazohusiana na ukatili
wa Kijinsia kuhakikisha wanazingatia miiko na misingi ya taaluma zao
kuhakikisha hawawi sehemu ya kuvuruga ushaidi.
“Sisi kama Wizara tutakapobaini
kwamba mtoa huduma wa Afya yoyote atakayeshiriki katika katika kosa la
kuvuruga ushaidi kwa waanga wa ukatili wa kijinsia hapa Nchini
tutamfutia lesseni ya kufanya kazi ya kutoa huduma za Afya katika Nchi
yetu’’. Aliongeza Dkt. Ndugulile.
Pamoja na masuala ya ukatili wa
Kijinsia Dkt. Ndugulile amesema pia vijana wengi wanaanza kujamiina
wakiwa katika umri mdogo na kwa mjibu wa takwimu za masula ya ukimwi za
mwaka 2017 zinaonesha asilimia 40 ya Watanzania ni vijana na kati hao
mabinti peke yake ni 80%.
Kufuatia hali hiyo ya vijana
kujihusisha na masuala ya kujiimiana Dkt. Ndugulile amesema serikali
inakusudia kupeleka Sheria Bungeni ili kupunguza umri wa vijana kuanzia
miaka 15 kupima umri kwa hiari lakini pia kujipima wenyewe na kuweza
kujilinda lakini pia kulinda wenzi wao.
Aidha Dkt. Ndugulile ameongeza
kuwa sheria iliyopo inasema mtoto chini ya umri wa miaka 18 harusiwi
kupima virusi kwa hiari labda kwa ruhusa ya mzazi wake lakini wiki ijayo
Wizara inapeleka bungeni mabadiliko ya sheria ili suala la kupima
virusi kwa hiari lianze kufanyika mpaka umri wa miaka 15 kwa kuwa watoto
sasa wanaanza kujiamiina katika umri huo na bila idhini ya wazazi.
Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa
Takwimu za Viashiria vya Hali ya Afya Nchini zinaonesha kwamba kati ya
27% ya mabinti walio katika umri wa miaka 15-19 mmoja kati ya watatu ama
ni mjazito au ana mtoto hii inatoa picha kwamba watoto hawa wanaanza
ngono katika umri mdogo ndio maana serikali inatoa chanjo ya kansa ya
mlango kizazi kwa watoto wa kike wenye umri huo lakini pia sula
limepelekea kufanyika kwa marekebisho ya sheria ili wapime virusi kwa
hiari.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Bw. Peter Serukamba
amewataka Wajumbe wa Kamati yake kuwa mabarozi wa masuala ya ukatili wa
Kijinsia Nchini ili masuala hayo yaweze kupewa kipaumbele katika Bajeti
za Wizara mbalimbali Serikalini.
Pamoja na maoni yake hayo Bw.
Serukamba ameyataja matendo ya ukatili kuwa yamekuwepo kwa mingi lakini
Jamii kama zilivyo mila na desturi zetu imukuwa ikifanya vitendo hivyo
kwa usiri tofauti na wenzetu wa Nchi za Magharibi ambapo watu
wanajitangaza hadharani kuwa ni wao ni mashoga na wanaweza kujitokeza
hata kugombea nafasi za juu katika uongozi.
Aidha kiongozi huyo wa Bunge
ameongeza kuwa pamoja na uwepo wa sheria mbalimbali lakini haitoshi tu
kutokomeza matendo haya hivyo kuitaka Wizara pamoja na wadau kutoa elimu
ya kutosha kwa umma ikiwemo adhabu kwa wote wanaohusika na makosa haya
kupewa adhabu kali.
Bw. Serukamba ameutaja umasikini
kuwa sababu mojawapo ya kuchochochea ukatili wa kijinsia kwa wanawake
kwa kuwa baadhi ya wanawake wanakubali kunyanyaswa kwasababu ya
umasikini wa kipato na utegemezi hivyo kukubali kupigwa au kuonewa kwa
namna mbalimbali.
Semina ya wabunge kuhusu Mpango wa
Taifa wa Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto
(MTAKUWA) imemalizika leo Jijijini Dodoma na imelenga kujenga uelewa
kwa kamati ya Bunge kuhusu masuala ya ukatili na mpanga mkakati huo wa
miaka mitano unaotegemea kukamilika mwaka 2022.
0 comments:
Post a Comment