NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
MKURUGENZI
Mtendaji wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE), Dkt. Aggrey Mlimuka amewaambia
waajiri nchini kuwa kujisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi sio hiari bali
ni lazima.
Dkt.
Mlimuka ameyasema hayo Alhamisi Novemba 28, 2019 jijini Dar es Salaam wakati
akifungua mafunzo ya siku moja yaliyoandaliwa na ATE na kuwaleta pamoja waajiri
kutoka sehemu mbalimbali nchini ili kujifunza kuhusu masuala ya Fidia kwa
Wafanyakazi.
“Naomba
tuelewane toka mapema, siyo hiari kujiunga na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi
hilo ni takwa la kisheria Mfuko huu uko pale kisheria na ni vema likaeleweka
mapema.”Alisema Dkt. Mlimuka
Alisema
Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) kiko kwa maslahi ya waajiri lakini pia kwa
maslahi ya waajiriwa (wafanyakazi) kwani wameajiriwa ili kufanya shughuli
mbalimbali na wanaweza kuumia au kupatwa na madhara yoyote wakati wakitekeleza
majukumu yao na ndio maana upo Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ambao umeundwa
maalum kushughulikia masuala hayo.
“Niwashukuru
sana viongozi wa WCF kwa kuja hapa leo
kutupatia mafunzo, sisi waajiri tutanufaika
vya kutosha na mafunzo haya ambayo yataweza kujibu maswali yaliyo mengi kutokana
na changamoto mbalimbali.” Alibainisha Dkt. Mlimuka.
Alisema,hapo
zamani malipo ya Fidia kwa Mfanyakazi aliyeumia yalikuwa kidogo sana, na ndio
maana Serikali ikaanzisha Mfuko huu ambao umesaidia sana katika kutatua
changamoto zilizokuwa zikitukabili kutokana na masuala ya Fidia.
Akizungumza
kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini,
Dkt. Abdulsalaam Omary alisema, Waajiri wanao wajibu wa kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wao
unapewa umuhimu wa kwanza na ndio maana WCF inatoa elimu mara kwa mara.
“Ifahamike
kuwa sisi WCF wajibu wetu wa msingi ni kulipa fidia stahiki na kwa wakati kwa
mfanyakzi aliyeumia, kuugua au kufariki wakati akitekeleza wajibu wake wa kazi… kusajili na kupokea michango kutoka kwa waajiri walio katika
sekta ya umma na binafsi Tanzania Bara, lakini pia tunalo jukumu la kisheria la
kukuza mbinu za kuzuia ajali na vifo kazini kwa kutoa elimu kwa waajiri lakini
pia wafanyakazi wenyewe na hiki ndicho tunachokifanya hapa leo.” Alisema
Dkt. Omary wakati akiwasilisha mada yake ya namna ya kudai Fidia.
Washiriki
hao walipatiwa mafunzo mbalimbali yakiwemo Sheria iliyoanzisha Mfuko,
Kujisajili na jinsi ya kuwasilisha michango WCF na namna ya kuwasilisha madai
ya Fidia, lakini pia Mafao yanayotolewa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE), Dkt. Aggrey Mlimuka, akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo kuusu masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi yaliyotolewa kwa Waajiri kutoka sehemu mbalimbali nchini na kufanyika jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2019.
Bw, Deo Ngowi kutoka kitengo cha Sheria Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), akiwasilisha mada kuhusu Sheria iliyoanzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi.
Bw.Pascal Rischard kutoka Kitengo cha Usajili na Uwasilishaji Michango WCF, akiwasilisha mada kuhusu namna ya kujisajili na kuwasilisha michango kupitia Portal ya WCF
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary, |
Meneja Madai Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bi. Rehema Kabongo, akiwasilisha mada kuhusu Mafao yatolewayo na WCF. |
Baadhi ya washiriki w asemina wakifuatilia mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki w asemina wakifuatilia mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki w asemina wakifuatilia mafunzo hayo.
Maafisa wa juu wa WCF, kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, Bi. Laura Kunenge, Bw. Deo Ngowi kutoka Kitengo cha Sheria na Bw. Pascal Richard kutoka Kitengo cha Usajili na Uwasilishaji Michango WCF
Baadhi ya washiriki w asemina wakifuatilia mafunzo hayo.
0 comments:
Post a Comment