Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akieleza jambo kwa Wanakamati ya
Maandalizi alipotembelea Uwanja wa Ilulu kukagua maandalizi ya Mbio za
Mwenge wa Uhuru zinazotarajiwa kufanyika Mkuani Lindi. Kushoto ni Mkuu
wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe.
Godfrey Zambi akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea uwanja wa Ilulu kukagua
maandalizi ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru. Kulia ni Katibu Mkuu
Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Andrew Massawe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na watoto wa halaiki
alipowatembea kwa ajili ya kukagua maandalizi yao kuelekea Kilele cha
Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Sehemu ya watoto wa halaiki
wakifanya mazoezi ya utayarisho kuelekea Kilele cha mbio za mwenge wa
Uhuru zinazotarajiwa kufanyika Mkoani Lindi Oktoba 14, 2019.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akipokea mwamvuli kutoka kwa Meneja
wa Kampuni ya Simu ya Airtel Tanzania kanda ya Lindi Bw. Zephania
Ludigija itakayotumiwa na Watoto wa Halaiki.
PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
0 comments:
Post a Comment