Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya
Mtoto kutoka Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi. Mwajuma
Magwiza akizungumza na wadau na waandishi wa habari za Watoto na Malezi
wakati wa Kongamano kuhusu Ajenda ya kitaifa ya wajibu wa wazazi na
walezi katika malezi na matunzo ya familia liliwahusisha wahariri na
waandishi wa habari za Watoto na Familia lililofanyika jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya
Maendeleo ya Mtoto sehemu ya Familia kutoka Wizara ya Afya, Idara Kuu
ya Maendeleo ya Jamii Bi. Tausi Mwilima akizungumza kuhusu Agenda ya
Malezi na Makuzi kwana wadau na waandishi wa habari za Watoto na Malezi
wakati wa Kongamano kuhusu Ajenda ya kitaifa ya wajibu wa wazazi na
walezi katika malezi na matunzo ya familia liliwahusuha wahariri na
waandishi wa habari za Watoto na Familia lililofanyika jijini Dar es
Salaam.
Kaimu Naibu Mwakilishi wa Shirika
la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto Duniani UNICEF Bw. Francis
Odhiambo akielezea kwa wadau na waandishi wa habari za Watoto na Malezi
jinsi shirika hilo linavyosaidia kuhakikisjha jamii inapata elimu
sahihi ya malezi na makuzi ya familia wakati wa Kongamano kuhusu Ajenda
ya kitaifa ya wajibu wa wazazi na walezi katika malezi na matunzo ya
familia liliwahusisha wahariri na waandishi wa habari za Watoto na
Familia lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka
Wizara ya Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bw. Emmanuel Burton
akitoa somo la malezi na matunzo ya familia wakati wa Kongamano kuhusu
Ajenda ya kitaifa ya wajibu wa wazazi na walezi katika malezi na matunzo
ya familia liliwahusisha wahariri na waandishi wa habari za Watoto na
Familia lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Mtayarishaji wa
vipindi vya Watoto kutoka ITV Bi. Domitila Urassa akichangia mada katika
Kongamano kuhusu Ajenda ya kitaifa ya wajibu wa wazazi na walezi katika
malezi na matunzo ya familia liliwahusisha wahariri na waandishi wa
habari wa habari za watoto na familia lililofanyika jijini Dar es
Salaam.
Mmiliki na Mhariri Mkuu wa Mtandao
wa Fullshangwe Blog Bw. John Bukuku akichangia mada katika
Kongamano kuhusu Ajenda ya kitaifa ya wajibu wa wazazi na walezi katika
malezi na matunzo ya familia liliwahusisha wahariri na waandishi wa
habari wa habari za watoto na familia lililofanyika jijini Dar es
Salaam.
Baadhi ya
waandishi wa Habari wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa katika
Kongamano kuhusu Ajenda ya kitaifa ya wajibu wa wazazi na walezi katika
malezi na matunzo ya familia liliwahusuha wahariri na waandishi wa
habari wa habari za watoto na malezi liliofanyika jijini Dar es Salaam.
Picha Zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
******************************
Na Mwandishi Wetu
Wazazi na Walezi
nchini wameaswa kuzingatia suala la malezi kwa watoto katika familia
kwani bado ni changamoto na limekuwa likileta matatizo mbalimbali kwa
watoto nchini ikiwemo kukosa malezi bora kutoka kwa wazazi wao na wengi
wao kukimbilia kuishi mitaani.
Hayo yamebainika
leo jijini Dar e salaam katika kongamano la kitaifa la waandishi wa
habari kuhusu Agenda ya Kitaifa kuhusu wajibu wa wazazi/ walezi katika
malezi na matunzo ya Familia liliwakutanisha wahariri na waandishi wa
habari zinazohusu Watoto, Malezi na Matunzo ya Familia.
Akizungumza kwa
niaba ya Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy
Mwalimu, Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Mtoto BI. Mwajuma Magwiza
amesema kuwa Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Wizara kwa
kushirikiana na wadau kwa kipindi cha Disemba 2017 hadi Januari 2018
katika Halmashauri 12 za Ilala, Kinondoni, Temeke, Kigamboni, Ubungo,
Arusha, Iringa, Mbeya jiji, Wilaya ya Mbeya, Dodoma, Nyamagana na
Ilemela iligundua uwepo wa Jumla ya watoto 6,393 ikiwa watoto wa kike
1,528 na watoto wa kiume 4,865 wanaosihi na kufanya kazi mitaani.
Bi. Mwajuma
Magwiza ameongeza kuwa kati yao watoto 1,385 watoto wa kike 410 na
watoto wa kiume 975 walitambuliwa wakiishi na kufanya kazi mitaani muda
wa usiku uwepo wa watoto hawa maeneo ya mitaani kwa kiasi kikubwa
unatokana na kutowajibika kwa familia katika kumudu majukumu yao ya
kutunza na kulea watoto wao.
Aidha Bi.
Mwamjuma aliongeza kuwa kulingana na Taarifa ya utafiti wa afya ya mama
na mtoto na viashiria vya malaria ya mwaka 2015/16 inaonesha kwamba
asilimia 25 ya kaya za mijini na asilimia 27 ya kaya za vijijini zina
watoto ambao hawaishi na wazazi wao japokuwa mzazi mmoja au wote wawili
bado wapo hai, hii inamaana wanaishi katika familia pana au wao wenyewe
peke yao hivyo kukosa malezi ya wazazi wa pande zote mbili yaani baba na
mama katika makuzi yao.
”Hii inawaathiri
sana watoto kisaikolojia na wakati mwengine inasababisha na kuchangia
kwa kiasi kikubwa watoto kuamua kuondoka na kwenda maeneo mengine
ikiwemo mitaani, kujishughulisha na shughuli hatarishi kwa ajili ya
kujipatia mahitaji yao.” alisema Bi. Mwajuma.
Ameongeza kuwa
kwa kuthamini na kutambua umuhimu wa Familia katika malezi na matunzo ya
familia Serikali imendaa Ajenda hiyo ya Kitaifa ambayo inalenga katika
kuhakikisha kuwa wazazi na walezi na jamii kwa ujumla inakumbushwa na
kuhimizwa kuwajibika katika kuwapa matunzo na malezi bora watoto kwa
kuwajenga katika maadili, elimu ili waweze kufikia ndoto zao na kuwa na
taifa bora.
“Niwaombe
wamiliki wa vyombo vya habari kutenga muda wa kuwa na vipindi mahsusi
vya kuwakumbusha na kuwaelimisha wazazi na walezi wajibu wao katika
kuwalea, kuwatunza, kuzungumza na kuwapa upendo watoto ili kuhakikisha
kuwa watoto wetu wanakuwa salama na kufikia ndoto zao na kuja kuwa
wazazi bora wa baadae” alisema Bi. Mwajuma
Akizungumza kwa
niaba ya katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Mkurugezi Msaidizi
sehemu ya Familia kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii
Bi. Tausi Mwilima amesema kuwa katika kuhakikisha kuwa familia inasimama
imara na kutimiza wajibu wake katika kutoa malezi chanya Wizara
imeandaa Ajenda hii ya Kitaifa ambayo inaweka msisitizo katika maeneo
makuu 5 ambayo ni matunzo, ulinzi, mawasiliano, kujenga familia na
upendo.
Maeneo hayo yakieleweka na kufanyiwa kazi watoto na vijana wetu
watakuwa salama katika maeneo mbalimbali na tutaweza kutengeneza kizazi
bora na imara chenye watu wenye maadili na uzalendo kwa Taifa letu.
Ameongeza
kuwa Katika Kongamano hilo watatoka na mpango kazi wa pamoja wa namna
bora ya kutekeleza Ajenda hii kupitia vipindi mbalimbali ambapo Wizara
kwa kushirikiana na vyombo vya habari watakubaliana, namna bora ya
kutekeleza kampeni ya Familia Imara Taifa Bora itakayotekelezwa kwa
pamoja na wadau mbalimbali kupitia vyombo vya habari na njia nyingine
zitakazoonekana zinafaa kufikisha hamasa hii kwa jamii ili kuleta
matokeo chanya.
“Wizara
imejipanga katika kuhakikisha kuwa elimu hii inawafikia wadau mbalimbali
makundi maalum ya kimkakati, aidha, kwa leo tumeanza na kundi la
wanahabari watakaoshirikiana na Serikali katika kuhakikisha kuwa Ajenda
hii inatekelezwa na kila mtu vikiwemo vyombo vya habari”.alisisitiza Bi.
Tausi
0 comments:
Post a Comment