Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na
Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo ili kuweka jiwe la msingi ujenzi wa
Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tunduma katika eneo la Mpemba Tunduma
mkoani Songwe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua sehemu ya majengo
ya Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tunduma katika eneo la Mpemba
Tunduma mkoani Songwe.
Ujenzi wa majengo ya Hospitali ya
Halmashauri ya Mji wa Tunduma katika eneo la Mpemba Tunduma mkoani
Songwe ukiwa katika hatua za mwisho.
Mfano wa hospitali hiyo ya Halmashauri ya Mji wa Tunduma utakavyokuwa mara baada ya kukamilika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na
Viongozi wengine kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa
barabara ya Mpemba-Isongole km 50.3 itakayojengwa kwa kiwango cha lami.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi
wakati akiwasili Mpemba mkoani Songwe .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mtoto
Joan Schinga mmoja wa wanakwaya ya Watoto ya Light Angels ya Kanisa la
Moravian Tunduma ambao waliimba wimbo wa kukemea Rushwa mara baada ya
uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa barabara ya Mpemba-Isongole km
50.3 itakayojengwa kwa kiwango cha lami.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa
Mpemba mkoani Songwe mara baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa
barabara ya Mpemba-Isongole km 50.3 itakayojengwa kwa kiwango cha lami.
Wananchi wa Mpemba wakiwa katika
shamrashamra za mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika eneo hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa
Mbozi wakati akielekea Mpemba mkoani Songwe.
Wanakwaya ya Light Angels ya
Kanisa la Moravian Tunduma mkoani Songwe wakiimba wimbo maalum wa
kukemea Rushwa katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa
barabara ya Mpemba-Isongole km 50.3 itakayojengwa kwa kiwango cha lami.
PICHA NA IKULU
0 comments:
Post a Comment