![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/N-1-2.jpg)
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/N-2-2.jpg)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masula ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akihutubia vijana wakati wa mdahalo
wa miaka 20 ya kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere
uliofanyika kwenye ukumbi wa Sea View, Mkoani Lindi.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/N-3-2.jpg)
Baadhi ya Vijana wakimsikiliza
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masula ya Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo
pichani) wakati wa mdahalo wa miaka 20 ya kumbukizi ya Baba wa Taifa
Mwl. Julius Kambarage Nyerere uliofanyika Mkoani Lindi.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/N-4-2.jpg)
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/N-5-2.jpg)
Sehemu ya viongozi wakifuatilia
mada zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mdahalo wa miaka 20 ya
kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere uliofanyika
kwenye ukumbi wa Sea View, Mkoani Lindi. Katikati ni Katibu Mkuu, Chama
Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/N-6-2.jpg)
Mama Gertrude Mongela akiwasilisha mada kuhusu Miaka 20 bila Baba wa Taifa wakati wa mdahalo huo uliofanyika Mkoani Lindi.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/N-7-2.jpg)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masula ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akifuatilia mada iliyokuwa
ikiwasilishwa na Mama Gertrude Mongela kuhusu Miaka 20 bila Baba wa
Taifa wakati wa mdahalo huo. (Wa pili kutoka kushoto) ni Waziri wa
Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Ali Abeid Karume na
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony
Mavunde. Kulia ni Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/N-8-1.jpg)
Baadhi ya washiriki kwenye mdahalo
huo wakifuatailia mada zilizokuwa zinawasilishwa. Kulia ni Mkurugenzi
wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba. (Wa pili kutoka
Kushoto ni Mjukuu wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/N-9-1.jpg)
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/N-10-1.jpg)
Wawasilishaji Mada wakisikiliza
hoja zilizokuwa zikichangiwa na baadhi ya washiriki wakati wa mdahalo
huo wa kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius
Kambarage Nyerere uliofanyika kwenye ukumbi wa Sea View, Mkoani Lindi.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/N-11-1.jpg)
Kijana mmoja wapo aliyeshiriki mdahalo huo akichangia mada kuhusu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
………………………
Na; Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amewataka vijana nchini kuenzi na
kuziishi fikra na mitazamo za Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage
Nyerere kwa kuendeleza umoja uliopo nchini.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa
Kongamano la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Mkoani Lindi Oktoba 13, 2019,
Waziri Mhagama alisema kuwa vijana wanapaswa kuendeleza mambo mema yote
aliyoyafanya Baba wa Taifa enzi za uhai wake ili waendelee kujivunia juu
ya misingi ya amani na umoja iliyopo nchini.
“Vijana mna kila sababu ya
kujivunia amani na umoja ulipo katika taifa letu kwa kuwa Mwalimu
Nyerere alikuwa kiongozi aliyewapenda watu wote bila kujali imani zao
wala itikadi zao, alikuwa mzalendo na alitaka watanzania wote waishi kwa
umoja,” alisema Mhagama.
Aidha alifafanua kuwa, Amani na
umoja zilikuwa ni miongoni mwa tunu na falsafa kuu za Baba wa Taifa
ambayo ndiyo matokeo ya umoja na mshikamano wa taifa uliopo sasa.
Aliongeza kuwa miongoni mwa mambo
muhimu ambayo Baba wa Taifa alikuwa akisisitiza katika kuwaunganisha
watanzania ni pamoja na kulijengea uhuru taifa na watu watu wake,
kudumisha amani, upendo, umoja, uzalendo, mshikamano na kuandaa sera za
kukabiliana na ujinga, umaskini na maradhi.
Pamoja na hayo alisisitiza pia
vijana na wananchi kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya
kuendeleza maono ya Baba wa Taifa ikiwemo mageuzi ya kiuchumi yenye
manufaa kwa taifa.
Akitolea mfano sekta ya elimu
ambayo serikali ya awamu ya tano imekuwa ikitoa elimu bure ilikuwa ni
falsafa ya Mwalimu katika kuwajenga watanzania fikra ya kujitegemea ili
waweze kuukabili umasikini.
Waziri Mhagama alitumia fursa hiyo
pia kuwahimiza wananchi kuendeleza maudhui ya Mwenge wa uhuru ambao
umesaidia kwa kiasi kikubwa kuwaunganisha watanzania na kuwahamasisha
kufanya kazi kwa bidii ili wajiletee maendeleo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Lindi, Mhe. Godfrey Zambi alisema kuwa Mwalimu Julius Nyerere ataendelea
kukumbukwa na Watanzania kwa mchango wake aliojitolea katika kulijenga
taifa.
0 comments:
Post a Comment