Baadhi
ya wananchi wa vijiji vya Mrito na Kibaso katika tarafa ya Ingwe wilaya
ya Tarime mkoa wa mara wakinyoosha mikono kuunga mkono jitihada za
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Mendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
kwenda kutatua mgogoro wa takriban miaka 29 kati ya vijiji hivyo jana.
Mwananchi
wa kijiji cha Mrito wilaya ya Tarime Raphael Mwita akimkabidhi nyaraka
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
wakati wa kutafuta suluhu ya mgogoro wa muda mefu kati ya vijiji vya
Mrito na Kibaso mkoani jana.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
akizungumza na timu iliyoteuliwa na pande zenye mgogoro wa mpaka kati ya
vijiji vya Mrito na Kibaso wilaya ya Tarime mkoa wa Mara wakati wa
kutafuta suluhu ya mgogoro wa mpaka kati ya vijiji hivyo jana (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
…………………….
Na Munir Shemweta, WANMM TARIME
Naibu
waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
ameagiza timu ya Wataalamu wa sekta ya ardhi iende katika tarafa ya
Ingwe wilaya ya Tarime mkoa wa Mara kwenda kubainisha mipaka ya
kiutawala kwa ajili ya kutatua mgogoro wa muda mrefu wa mipaka baina ya
kijiji cha Mrito na Kibaso.
Uamuzi
huo Dkt Mabula unafuatia jitihada za kutafuta suluhu ya mgogoro huo kwa
njia ya mazungumzo kati ya pande hizo mbili kukwama kutokana na kila
upande kudai sehemu ya eneo la kijiji cha Mrito liko upande wake.
Kwa
mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi, timu hiyo itahusisha wataalamu wa sekta
hiyo kutoka ofisi ya Ardhi Kanda ya Simuyu na wale wa ofisi ya mkoa wa Mara badala ya Tarime kufuatia baadhi yao kutuhumiwa na pande hizo kuwa wamekuwa wakichangia kuendelea kwa mgogoro baina ya vijiji hivyo.
Hata
hivyo, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alishangazwa
kusikia kutoka kwa wananchi wa vijiji vya Mrito na Kibaso kuwa ndani ya
kijiji kimoja kuna viongozi wawili wa kijiji jambo alilolieleza kuwa
suala hilo halikubaliki.
Dkt
Mabula alibainisha kwa kusema kuwa, zoezi hilo litakalohusisha pia
wananchi kumi kutoka kila upande wa vijiji vyenye mgogoro litafanyika
kwa muda wa siku mbili na kusisitiza kuwa lengo ni kumaliza kabisa
mgogoro huo uliodumu kwa takriban miaka 29.
Alisema,
baada ya kukamilika kwa zoezi la kubainisha mipaka ya kiutawala taarifa
yake itawasilishwa kwa mkuu wa wilaya ya Tarime mkoani Mara Mtemi
Msafiri ambaye jumanne ijayo tarehe 22 Oktoba 2019 atatakiwa kuwaeleza
wananchi wa vijiji hivyo makubaliana yatakayofikiwa kwa nia ya kumaliza
mgogoro huo.
Awali
kulikuwa na mabishano makali ya pande zinazopingana katika mgogoro huo
ambapo wananchi wa kijiji cha Mrito walidai wenzao wa Kibaso wamevamia
eneo lao huku wale wa Kibaso wakidai sehemua ya eneo linalodaiwa ni la
Mrito ni la kwao.
Joseph
Mangure aliyekuwa Mwenyekiti wa kijiji cha Mrito tangu mwaka 2009 hadi
2014 alisema sehemu ya eneo la kijiji cha Mrito inayodaiwa na wananchi
wa Kibaso kuwa ni la kwao siyo sahihi kwa kuwa kijiji cha Mrito kina
nyaraka zote zinazoonesha mipaka yake tofauti na wananchi wa Kibaso
alioeleza kuwa hawana Nyaraka zinazoonesha uhalali wa eneo lake.
Naye
Diwani wa Kata ya Bihanja wilayani Tarime Mustafa Masiani alieleza kuwa
suluhu pekee ya mgogoro baina ya vijiji hivyo ni kwa viongozi wa
serikali za vijji husika kukaa pamoja na na
kutafuta suluhu ya mgogoro na kubainisha kuwa tatizo lililopo ni baadhi
ya wananchi kuufanya uongozi wa vijiji kama uongozi wa Koo.
0 comments:
Post a Comment