
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akivishwa skafu na Daniel Ngwema Mara
baada ya kuwasili katika uwanja wa Mpira wa Kilimahewa kwa ajili ya
kushuhudia fainali ya timu ya Nyakahanga dhidi ya timu ya Magambo
katika mashindano ya ligi ya Bashungwa Karagwe Cup iliyofanyika katika
wilaya ya Karagwe mkoani Kagera. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa wilaya
hiyo, Mhe.Godfrey Mweruka akiwa pamoja na Waziri wa Biashara na Viwanda,
Mhe.Innocent Bashungwa.

Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa ameongozana na Mkuu wa wilaya ya
Karagwe, Godfrey Mweruka akisalimiana na wachezaji wa timu Nyakahanga
kabla ya mchuano huo kuanza katika uwanja wa Kilimahewa uliopp katika
wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.

Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akimkabidhi zawadi ya cheti mshangilia
bora wa mashindano ya Ligi ya Bashungwa Karagwe Cup kabla kufunga
mashindano hayo.

Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akisaini kitabu cha wageni Mara baada ya
kuwasili katika uwanja wa Kilimahewa kushuhudia mechi kati ya timu ya
Nyakahanga ambayo imeibuka kidedea katika ya timu ya Nyakahanga na
Magambo. Wa pili Julia ni Waziri wa Biashara na Viwanda, Mhe.Innocent
Bashungwa.

Baadi ya umati wa wakazi wa
Karagwe waliojitokeza kushuhudia mechi kati ya Nyakahanga na Magambo
ambapo Nyakahanga iliibuka kidedea kwa mikwaju ya penati.

Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu( Julia) akizungumza na mamia ya wananchi
waliojitokeza kushuhudia fainali ya mechi kati ya Nyakahanga na Magambo
kabla ya kufunga ligi ya mashindano ya mpira wa miguu wa Bashungwa
Karagwe Cup.

Vijana wa skauti wakipiga paradi mbele ya mgeni rasmi kabla ya fainali ya Bashungwa Karagwe Cup kuanza.

Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa na viongozi wa mkoa
wa Kagera wakiwa wameshika kombe kwa ajili ya kumkabidhi timu ya
Nyakahanga iliyoibuka kidedea katika Mashindano ya Ligi ya Mpira wa
miguu ya Bashungwa Karagwe Cup.
( Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)
**********************************
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amefunga Mashindano ya
ligi ya mpira wa miguu ya Bashungwa Karagwe Cup ambapo timu ya
Nyakahanga imeibuka kidedea dhidi ya timu ya Magambo.
Akizungumza kabla ya
kufunga mashindano hayo, Mhe.Kanyasu amewataka vijana kuitangaza
Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato kupitia michezo
Naye, Waziri wa
Biashara na Viwanda Mhe.Innocent Bashungwa ambaye ni Mbunge wa Karagwe
na Mratibu wa Mashindano hayo amesema umati wa watu waliojitokeza
kushuhudia Mashindano hayo ni ishara tosha ya umoja na mshikamano wa
wakazi wa Karagwe kwa Mbunge wao
0 comments:
Post a Comment