![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/PICHA-1-2.jpg)
Ofisa Mafunzo Kitengo cha Masoko
wa Kampuni ya Uwekezaji UTT-AMIS, Waziri Ramadhan, akitoa elimu ya
Uwekezaji wa Pamoja kwa wafanyabiashara ndogondogo na vijana, eneo la
Ilala, jijini Dar es Salaam.
……………….
Na Mwandishi Wetu
OKTOBA 14, mwaka huu, Tanzania imeadhimisha miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Katika uhaki wake, Mwalimu Nyerere
alikuwa na sifa ya utu, mpenda maendeleo, hakupenda kuona watu
wakinyanyaswa, wakionewa au kupuuzwa kwa sababu za unyonge wao.
Mwalimu Nyerere alichukia rushwa,
ufisadi, wizi na aina zote, kujenga misingi imara ya kulifanya Taifa
lijitegemea, kutumi rasilimali zilizopo ili kujiletea maendeleo ya
kweli.
Pia Mwalimu Nyerere alipenda kuona
taasisi zilizoanzishwa na serikali zikiwakomboa Watanzania katika
nyanja mbalimbali ili waweze kukuza mitaji, kipato chao na kulipa kodi
stahiki.
Miongoni mwa taasisi iliyobeba maono ya Mwalimu Nyerere na kuyafanyia kazi kwa vitendo ni UTT AMIS.
Taasisi hiyo ipo chini ya Wizara
ya Fedha na Mipango iliyopewa dhamana ya usimamizi wa mali kupitia
Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja.
Utajiri siyo fedha ambazo mtu
anakusanya bali ni fedha zinazowekwa na kufanya kazi. Tamaduni zetu
zimeifanya jamii kubwa kuhifadhi fedha ndani katika vyungu, magodoro,
vibubu.
Uwekaji akiba na uwekezaji ni dhana mbili tofauti. Uwekaji akiba ni mzuri lakini bila kuziwekeza ni bure.
Ili uwe muwekaji akiba mzuri, unapaswa kuwa na nidhamu ya kujizoesha muda mrefu.
Awali UTT AMIS ilipewa dhamana ya
usimamizi wa mifuko mitano ambayo ni Mfuko wa Umoja, Wekeza Maisha,
Watoto, Mfuko wa Kujikimu na Mfuko wa Ukwasi. Hivi sasa taasisi hiyo
imeongeza mfuko mwingine wa Hati Fungani.
Nchini Tanzania unaweza kuwekeza
fedha zako katika masoko ya fedha, mitaji. Hatua hiyo inahusisha akaunti
za muda maalum na zisizo za muda maalum katika benki za biashara.
Pia hati fungani za Serikali za
muda mfupi, mrefu, kampuni na hisa zilizoorodhosgwa katika Soko la Hisa
Dar es Salaam (DSE) ambazo zina nafasi kubwa ya kurejesha gawio zuri.
Uwekezaji unaofanywa na taasisi
hiyo kupitia mifuko ambayo wanaisimamia ni fursa mbadala inayowezasha
watu, vikundi, taasisi, kampuni kuwekeza pesa zao kwa Meneja wa UTT.
Meneja huzichukua fedha hizo, kuziwekeza kwenye masoko ya fedha, mitaji kulingana na waraka wa makubaliano.
Faida inayopatikana hugawanywa kwa wawekezaji kulingana na uwiano wa uwekezaji uliofanyika kwenye mfuko husika.
Mfuko wa Umoja, ulioanzishwa Mei
16, 2005 ukilenga kutimiza mahitaji tofauti ya wawekezaji. Awali bei ya
kipande ilikuwa sh. 70, kwa sasa sh. 590.2060.
Sifa zilizopo katika mfuko huo ni
vipande kuuzwa kwa thamani halisi (hakuna gharama za kujiunga). kiwango
cha chini cha kujiunga ni vipande 10 tu.
Malipo ya mauzo hutozwa asilimia
moja ya thamani halisi, pia ni rahisi kujiunga, kutoka ambapo manunuzi
na mauzo hufanyika kila siku ya kazi.
Mfuko wa Watoto una lengo la
kuwasaidia watoto katika maendeleo yao nchini. Awali bei ya kipande
ilikuwa sh. 100, mfuko ulianzishwa Oktoba 1, 2008.
Sifa za mfuko huo ni uwekezaji kwa
ajili ya mtoto mwenye umri chini ya miaka 18. Kiwango cha chini cha
uwekezaji sh. 10,000, unaruhusiwa kuwekeza kidogo kidogo kwa sh. 5,000.
Sifa nyingine ni vipande kuuzwa
kwa thamani halisi (hakuna gharama za kujiunga), mfuko hutoa mipango ya
aina mbili, kwanza malipo ya ada, pili mpango wa kukuza mtaji.
Malipo ya ada na mauzo ya vipande
yanaruhusiwa pale mtoto anapofikisha miaka 12. Mfuko huo ni miongoni mwa
mifuko inayotatua changamoto za kielimu hasa katika ulipaji ada kwa
wanafunzi, kutoa mtaji baada ya ukomo wa shule kufikia.
Pia mfuko una mipango miwili
mikubwa, mpango wa ada za shule na mtaji kwa mwanao. Ili mzazi aweze
kuchangia kupitia mfuko huo, anapaswa kuweka sh. 10,000 kima cha chini
na hakuna ukomo kwenye kiwango cha juu.
Mfuko ulianzishwa mwaka 2008. Kiwango cha chini cha kipande kilianzia sh. 100, hivi sasa sh. 346.3151.
Mfuko wa Jikimu una lengo la
kukidhi mahitaji ya wawekezaji wanaohitaji uhakika wa mapato ya mara kwa
mara, ulianzishwa Novemba 3, 2008 ukiwa na sifa za mipango ya
uwekezaji, kiwango cha uwekezaji, mpango wa gawio robo mwaka.
Kiwango cha chini cha uwekezaji
sh. milioni 2, mpango wa gawio wa mwaka (kiwango cha chini cha uwekezaji
sh. milioni moja), tatu mpango wa mwaka wa kukua (sh. 5,000).Vipande
vinauzwa kwa thamani halisi (hakuna gharama za kujiunga).
Mfuko wa Ukwasi unaotoa nafasi ya
uwekezaji mbadala kwa wawekezaji wakubwa au taasisi ambao wangependa
kuwekeza fedha zao za ziada kwa kipindi kifupi ama cha kati huku
wakikuza mtaji wao.
Ulianzishwa Aprili 30, 2013, bei ya kipande ikiwa sh. 100.00, hivi sasa imepanda sh. 126.3239.
Sifa za mfuko huo ni rahisi
mwekezaji kupata fedha zake za mauzo ya vipande ndani ya siku tatu za
kazi baada ya maombi ya kuuza vipande kupokelewa Makao Makuu ya UTT
AMIS.
Mfuko huo hauna ada ya kujitoa
wala kujiunga, una unafuu wa gharama za uwekezaji, unafaa kwa wawekezaji
mmoja mmoja au taasisi, kiwago cha chini cha kuwekeza sh. 5,000,000.00.
Kuongeza uwekezaji wako sh.
1,000,000.00, pia unaruhusu uhamishaji vipande kutoka kwa mwekezaji
mmoja kwenda mwingine, kuruhuusu uhamishaji vipande kwenda kwenye mifuko
mingine, kuviuza kwa thamani halisi.
Mfuko wa Wekeza Maisha unamwezesha mwekezaji kupata faida pacha (mapato mazuri pamoja na mafao ya bima).
Mfuko huo ulianzishwa Mei 16,2007,
wawekezaji kati ya miaka 18 na 55 ndio wanaoruhusiwa kujiunga. Unatoa
mipango ya aina mbili, kuchangia uwekezaji awamu ya kwanza, mkupuo
mmoja.
Vipande vinauzwa kwa thamani
halisi, hakuna gharama za kujiunga. Kujiunga ni sh. 8,340.00 tu kwa
mwezi. Bei ya kipande kwa sasa sh. 416.4499.
Mafao ya bima yanayopatikana ni bima ya maisha, ulemavu wa kudumu na bima ya ajali.
Mfuko unamwezesha mwekezaji
kuwekeza kwa mpangilio, kuchangia kwa mwezi, mara mbili kwa mwaka, mara
moja kwa mwaka ambapo faida za uwekezaji katika Mifukoya Uwekezaji wa
Pamoja ni kukuza mtaji kwa kutoa faida nzuri ukilinganisha na mifuko
mingine kwenye masoko ya fedha.
Faida nyingine ni kutawanya hatari
za uwekezaji, mwekezaji hupunguza athari za uwekezaji kwa kuwekeza
katika uwekezaji auai, wawekezaji kufaidika na unafuu wa gharama za
uwekezaji.
Pia wawekezaji wanaweza kufuatilia maendeleo ya masoko ya fedha kwa kufuatilia maendeleo ya mifuko.
Mfuko mpya Hati Fungani
unaojulikana kama ‘Bond Fund’ ni kati ya mifuko ya uwekezaji wa pamoja
inayoendeshwa na UTT AMIS ulioanzishwa kwa malengo maalum.
Kuanzishwa kwa Mfuko wa Hati
Fungani kumetokana na mahitaji ya wawekezaji na uchambuzi wa bidhaa za
kifedha zilizoko kwenye soko la mitaji kwa sasa.
Mfuko utawawezesha wawekezaji
wadogo na wa kati kuzifikia fursa za uwekezaji ambazo kwa hali ya
kawaida ni wawekezaji wachache na wakubwa ndio wanaozifikia.
Pia utawekeza kwenye hati fungani
zilizoorodheshwa kwenye soko la hisa kwa asilimia 90 na asilimia 10
itakuwa kwenye uwekezaji wenye ukwasi mkubwa.
Lengo ni kuwawezesha wawekezaji wanaohitaji kuchukua fedha kutokana na uwekezaji wao katika mfuko wafanye hivyo.
Mfuko umeundwa ili kumwezesha kila
mwekezaji kuchagua kama anapenda kukuza mtaji au kupokea gawio kwa
mwezi, kila miezi sita kutokana na mahitaji yake ya kifedha.
Akiuzungumzia mfuko huo,
Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS, Daudi Mbaga, alisema
umelenga kuondoa changamoto ambazo wawekezaji wanakutana nazo.
Anasema soko la fedha lina bidhaa nyingi zilizobuniwa ili kukidhi mahitaji tofauti ya watumiaji.
Baadhi ya bidhaa hizo zinaeleweka
kirahisi hata namna ya kuzifikia na kuwekeza lakijni wakati mwingine
hazitoi faida shindani kwa wawekezaji.
Anasema baadhi ya wawekezaji hasa
wadogo ni vigumu kuwekeza kwenye baadhi ya bidhaa katika soko la fedha.
Mfuko wa Hati Fungani umeratibiwa ili kuondoa changamoto hizo.
Mwekezaji anapata faida sawa na
wawekezaji wakubwa, akihitaji fedha anauza baadhi ya umiliki wake kwenye
mfuko kwa utaratibu rahisi bila kupoteza faida aliyoipata.
Pia mfuko huo unawafaa wawekezaji
wakubwa kwa sababu ya faida shindani, gharama ndogo za kuwekeza, ukwasi
wa kutosha, usalama wa mtaji, hatari ndogo za uwekezaji.
Mfuko unatoa fursa kwa wawekezaji kuwekeza, kushiriki katika masoko ya mitaji, kufaidika na uwekezaji huo.
Kwa mantiki hiyo, mfuko
umeandaliwa ili kutoa fursa kwa wawekezaji wa kipato cha chini, kati na
kipato cha juu ambao ni watu binafsi, kampuni, taasisi na vikundi rasmi
wanaweza kushiriki katika uwekezaji kwenye mfuko huo.
Mbaga anasema, mfuko una mipango miwili ya uwekezaji ili kukidhi matakwa tofauti ya wawekezaji.
Kuna mpango wa kukuza mtaji, gawio kila mwezi na gawio kila miezi sita, mpango wa kukuza mtaji.
Gawio la mara kwa mara
halitatolewa kwa wawekezaji badala yake faida iliyopatikana itarudishwa
kwenye uwekezaji wa awali kwa kununua vipande vitakavyonunuliwa kwa bei
ya wakati huo.
Mpango huo utawafaa wawekezaji
wanaohitaji kuweka akiba kwa malengo maalum mfano kujenga nyumba au
wafanyakazi wenye kipato kama wangependa kuwa na fedha ya akiba.
Wawekezaji katika mpango huo
wanaweza kuuza kiasi chochote cha uwekezaji wakiwa wamekidhi vigezo
vinavyohusu uuzwaji wa vipande.
Wawekezaji wanaohitaji kuchukua
faida kila mwezi kama wastaafu wanaopata fedha zao za mkupuo, kuwekeza
kwenye mfuko, wanashauriwa kuchagua kupokea gawio kila mwezi ili wapate
kipato cha kuishi bila kupoteza fedha walizopata.
Mbaga anasema wawekezaji wengine
wanaopata fedha nyingi mara moja mfano wachimba madini, wanaweza
kuchagua gawio kila mwezi ili wafanye shughuli zao bila kuathiri mtaji
wao.
Pia wawekezaji watakaojiunga na
mpango huo wanaweza kuuza vipande kidogo au vyote ili mradi wawe
wamekidhi vigezo vya mfuko vinavyohusu uuzwaji vipande.
Mpango wa gawio kila miezi sita,
Mbaga alisema hutegemea na mahitaji ya fedha ya mwekezaji na
anavyochagua kwenye fomu ya maombi ya kuwekeza kwenye mfuko.
Kwa wawekezaji ambao wanahitaji
kuchukua faida kila miezi sita mfano wafanyakazi wanaohitaji kuweka
kiasi cha fedha ili faida inayopatikana itumike kulipa ada kusomesha
watoto, wanaweza kuchagua kupokea gawio kila miezi sita.
Pia kuna wawekezaji wanaopata
fedha nyingi mara moja kama wakulima wa mazao mbalimbali ya msimu,
wanaweza kuchagua kupata gawio kila miezi sita.
Wawekezaji watakaojiunga na mpango huo wanaweza kuuza vipande kidogo au vipande vyote ili mradi wawe wamekidhi vigezo vya mfuko.
0 comments:
Post a Comment