Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation
for Civil Society (FCS), Francis Kiwanga, akitoa taarifa kwa waandishi
wa habari (hawapo pichani) kuhusu wiki ya Azaki ambayo itaanza Novemba
nne hadi nane mwaka huu na itazinduliwa na Mhe. Waziri Mkuu ,Kassim
Majaliwa,kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodma.
Mbunge
wa Viti Maalumu wa Mkoa wa Dodoma, Fatma Tawfiq ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Asasi ya Woman Wake Up,akisisitiza jambo kwa waandishi wa
habari (hawapo pichani) wiki ya Azaki ambayo itaanza Novemba nne hadi
nane mwaka huu na itazinduliwa na Mhe. Waziri Mkuu ,Kassim Majaliwa
,kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodma.
Mwakilishi wa Msajili wa Mashirika
yasiyokuwa ya kiserikali (NGOS), Charles Komba,akizungumza na waandishi
wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutoa taarifa kuhusu wiki ya Azaki
ambayo itaanza Novemba nne hadi nane mwaka huu na itazinduliwa na Mhe.
Waziri Mkuu ,Kassim Majaliwa,kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodma.
Mkurugenzi Mtendaji Haki
Rasiliamali,Rachel Chagonja,akizungumza na akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa kuhusu wiki ya Azaki
ambayo itaanza Novemba nne hadi nane mwaka huu na itazinduliwa na Mhe.
Waziri Mkuu ,Kassim Majaliwa,kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodma.
Sehemu ya waandishi wa habari wakifatilia
……………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
wiki ya asasi za Kiraia Tanzania [AZAKI] itakayofanyika jijini Dodoma
kuanzia Novemba 4 hadi 8 mwaka huu.
Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma
na Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Foundation for Civil Society [FCS]
BW.Francis Kiwanga amesema wiki ya asasi za kiraia nchini itakutanisha
zaidi ya asasi za kiraia 500 kutoka nchi nzima Tanzania bara na visiwani
Zanzibar.
Bw.Kiwanga amefafanua kuwa Wiki ya Asasi za Kiraia [AZAKI]
itajumuiya Maonesho ya kazi mbalimbali zinazofanywa na asasi hizo huku
lengo likiwa ni kuimarisha ubia kati ya asasi za kiraia na wadau
mbalimbali katika kutimiza azma ya kuiletea Tanzania Maendeleo.
“Lengo la kongamano hilo
nikuimarisha ubia kati ya asasi za kiraia na wadau mbalimbali katika
juhudi za kutimiza azma ya kuileteaTanzanaia maendeleo,” amesema .
Hata hivyo amesema “Kupitia kongamano hili asasi za kiraia
zitafanya majadilianao juu ya kazi zao, kubadilishana uzoefu na
kuona ni jinsi ambavyo zinaweza kushirikiana wenyewe kwa wenyewe na
wananchi, serikali, bunge, wabia wa Maendeleo na sekta binafsi,”
amesema.
Kwa upande wake, Mbunge wa Viti
Maalumu wa Mkoa wa Dodoma, Fatma Tawfiq ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Asasi ya Woman Wake Up,amewataka wananchi wa kada zote kuhudhuria
maonesho hayo ili kufahamu shughuli na umuhimu wa asasi hizo kwa
maendeleo ya jamii.
Mhe.Tawfiq amesema kuwa wanapaswa
kufahamu kuwa asasi za kiraia si adui wa serikali bali zinapaswa
kushirikiana pamoja katika kufitia azma ya kuwahudumia wananchi.
“Kuna dhana kwamba asasi za kiraia
hupokea fedha kutoka kwa wafadhili na kuzitumia isivyo, siyo kweli
ingawa inawezekana zipo chache zinafanya hivyo na hiyo haimaanishi kuwa
asasi zote zinafanya hivyo bali ni udhaifu wa watu au mtu binafsi,”
amesisitiza
Mwakilishi wa Msajili wa Mashirika
yasiyokuwa ya kiserikali (NGOS), Charles Komba,amesema kuwa serikali
inatambua umuhimu wa asasi hizo kwani zimekuwa msaidizi mkubwa kwa
maendeleo.
Aidha amesema kuwa asasi za kiraia zimesaidia kufikisha huduma katika maeneo ambayo ni nadra kwa serikali kuyafikia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Haki,Rasilimali ,Mafuta ,Madini na Gesi Rachel Chagonja amesema
taasisi hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kufanya tafiti mbalimbali
zinazohusiana na madini,Mafuta na gesi ambapo ni mchango mkubwa kwa
serikali Ya Tanzania.
Mwenyekiti wa Shirikisho la
Wenyeulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Ummy Ndeliyananga, amesema kuwa
kwenye wiki hiyo serikali pamoja na wadau wa masuala ya ulemavu
watajadili mwenendo wa utoaji fedha za mikopo kwa kundi hilo muhimu.
Hata hivyo amesema kuwa walemavu
wanapaswa kupewa mikopo hiyo ya asilimia mbili inayotengwa kwenye
halmashauri ili waweze kushiriki kuimarisha uchumi wananchi.
Afisa Uhusiano wa kituo cha sheria
na Haki za Binadamu,Legal Human Rights Centre[LHRC] Michael Malya
amesema katika wiki hiyo kituo hicho kitajihusisha na utoaji wa huduma
za kisheria.
Ikumbukwe kuwa FCS itatoa tuzo za Umahiri wa asasi za kiraia ili
kusheherekea na kutambua ufanisi na michango za taasisi na
watu binafisi katika uchocheaji na uimarishaji wa sera ya maendeleo ya
nchi.
Zaidi ya asasi za kiraia 15 zikishirikiana na FCS Kuandaa wiki ya
AZAKI ni LHRC,LSF,Save the children, Wajibu Institute,UN
Women,Oxfam,Twaweza,Policy Forum,msichana
Initiative,Hakirasilimali, UNA Tanzania, Acountability
Tanzania,Sikika,TLS,SHIVYAWATA,na TANGO.
Kaulimbiu wiki ya asasi za Kiraia [AZAKI] Mwaka ,2019 ni ubia kwa Maendeleo ,Ushirikiano kama chachu ya Maendeleo.
0 comments:
Post a Comment