
Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu (Uwekezaji), Angela Kairuki wakati alipowasili kwenye hoteli ya
Serena jijini Dar es salaam kumwakilisha Rais Dkt. John Pombe
Magufuli katika utoaji wa tuzo za Rais kwa viwanda vilivyofanya vizuri
kwa mwaka 2018, Oktoba 17, 2019. Katikati ni Waziri wa Viwanda na
Biashara, Innocent Bashungwa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akimkabidhi tuzo ya ushindi wa jumla, Satbir Singh Hanspaul ambaye ni
Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya HANSPAUL wakati alipomwakilisha Rais, Dkt.
John Pombe Magufuli katika utoaji wa tuzo za Rais kwa viwanda
vilivyofanya vizuri kwa mwaka 2018 kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es
salaam, Oktoba 17, 2019. Watatu kushoto ni Waziri wa Viwanda na
Biashara, Innocent Bashungwa na Kushoto ni Mwenyekiti wa Shirikisho la
Viwanda Tanzania (CTI), Subhash Patel.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza wakati alipomwakilisha Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika
utoaji wa tuzo za Rais kwa viwanda vilivyofanya vizuri kwa mwaka 2018
kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam, Oktoba 17, 2019. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa
katika picha ya pamoja na watoto Janainnah Salum (katikati), Fatma
Khery (kushoto) na Rahma Hassani ambao aliomba kupiga nao picha baada ya
kuvutiwa na sarakasi waliyoonyesha wakiwa na kikundi cha Safi cha
Bungoni jijini Dar es salaam katika utoaji wa tuzo za Rais kwa viwanda
vilivyofanya vizuri kwa mwaka 2018 zilizofanyika kwenye hoteli ya
Serena, Oktoba 17, 2019.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Shirikisho la
Viwanda Tanzania(CTI), Subhash Patel wakati alipowasili kwenye hoteli ya
Serena jijini Dar es salaam kumwakilisha Rais Dkt. John Pombe
Magufuli katika utoaji wa tuzo za Rais kwa viwanda vilivyofanya vizuri
kwa mwaka 2018, Oktoba 17, 2019. Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu (Uwezeshaji), Angela Kairuki. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)

0 comments:
Post a Comment