
Waziri wa Madini Doto Biteko kushoto, akijadiri jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John
Mongella akizunguza na wachimbaji wadogo wa dhahabu katika mkutano wa
hadhara katika machimbo ya Shilalo Wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza,
anaefuata ni Waziri wa Madini Doto Biteko na kutoka kulia ni Mbunge wa
Jimbo la Misungwi Charles Kitwanga.

Waziri wa Madini Doto Biteko
akiongea na wachimbaji wadogo wa dhahabu kwenye mkutano wa hadhara
katika machimbo ya Shilalo Wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza.

Waziri wa Madini Doto Biteko
akiongea na wachimbaji wadogo wa dhahabu katika mkutano wa hadhara
katika machimbo ya Shilalo Wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza.

Baadhi ya Wachimbaji wadogo wa Madini waliohudhulia katika mkutano wa hadhara ulio ongozwa na Waziri wa Madini Doto Biteko.
…………………
Na Tito Mselem Mwanza,
Waziri wa Madini Doto Biteko
ametatua mgogoro ulio dumu kwa muda mrefu na kuruhusu wachimbaji
waendelee na shughuli za uchimbaji katika Machimbo ya wachimbaji wadogo
ya Shilalo Wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza.
Mgogoro huo ulisababisha
shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu kusitishwa kutokana na sababu
za kimaslahi katika madura 38 kati ya 57 yaliyoko kwenye Machimbo hayo.
Shughuli za uchimbaji wa
madini ya dhahabu zilisitishwa Oktoba 7 mwaka huu na Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza, John Mongella, kwa muda usiojulikana kutokana na mgogoro wa
umiliki wa eneo yalipo mashimo hayo ili kuweka utaratibu wa usimamizi wa
mapato.
Akizungumza na wachimbaji
wadogo katika mkutano wa hadhara Waziri Biteko aliwataka waache fitina,
majungu na makundi huku akiwataka kufanya kazi na kushirikiana kwa
pamoja kwani lengo la Serikali ni kuwafanya wanufaike na uchumi wa
madini.
“Rais Dkt. John Pombe Magufuli
alituteuwa tufanye kazi kubwa mbili katika sekta ya madini, tuwapatie
wachimbaji wadogo maeneo ya kuchimba ili mshiriki kuinua uchumi wa nchi
na tuhakikishe mnalipa kodi za Serikali ili fedha hizo zisaidie
kuboresha maeneo mbalimbali kwa maslahi ya wananchi wote ikiwemo afya na
elimu”.
“Lazima mfanye shughuli zenu
kwa usalama lakini mtakapokuwa na migogoro hicho ni kiashiria cha
uvunjifu wa amani, Serikali hatuwezi kuruhusu watu wake wakaumizana
ndiyo maana Mkuu wa Mkoa alichukua jukumu la kusitisha shughuli za
uchimbaji kwa muda, tumeshirikiana tumetatua mgogoro huo hivyo
ninawasisitiza wachimbaji wote muachane na siasa zisizo na maana badala
yake mfanye kazi na mlipe kodi ya serikali,” alisema Biteko.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa
wa Mwanza, John Mongella, aliwataka wachimbaji na wamiliki wa eneo hilo
kuweka utaratibu wa usimamizi wa mapato ili kila mtu apate haki yake
anayostahili na anufaike kutokana na mapato yanayopatikana katika
machimbo hayo.
Aidha, Mmiliki wa eneo hilo
Wilbert Kukwanja, alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mongella kwa
kuwakutanisha na Waziri Biteko na kumaliza mgogoro huo kwa sababu
kusitishwa kwa shughuli za uchimbaji katika machimbo hayo kuliwaathiri
kiuchumi ambapo aliahidi kulinda amani katika eneo hilo na kutoruhusu
migogoro kutokea tena.
Naye, Mbunge wa Jimbo la
Misungwi, Charles Kitwanga aliwataka wachimbaji katika eneo hilo
kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia usalama wao kwanza pamoja na
kuepuka migogoro ambayo itawaletea hasara wao na familia zao endapo
serikali itasitisha shughuli za uchimbaji huku akiwasisitiza kulipa kodi
za serikali kila wanapozalisha.
Baadhi ya wachimbaji katika
eneo hilo akiwemo Ally Bushiri na Maige Gaude, walimshukuru Rais
Magufuli kwa kuteuwa viongozi wachapa kazi kama Biteko ambae ametatua
mgogoro huo kwani walikuwa wamekwishakata tamaa walidhani tatizo hilo
litadumu kwa muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi.
0 comments:
Post a Comment