Leo October 28, 2019 Naibu Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson ameongoza Kamati ya
Maazimio ya Semina ya Wajumbe wa Chama cha Wabunge Wanawake wa Mabunge ya Nchi
Wanachama wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika uliofanyika Mkoani Arusha.
Katika Semina hiyo iliyofunguliwa na
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan jana Oktoba 27, 2019 imepitisha
maazimio muhimu kwa mustakabali wa jumuiya hiyo.
Waazimio hayo ni pamoja na Mabunge
Wanachama wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika yatunge na kuhakikisha
zinatelekezwa sheria zitakazohakikisha vyama vya siasa vinazingatia usawa
katika nafasi za uongozi.
Kadhalika sheria zitakazozuia ama
kuadhibu makosa yanayohusiana na ukatili na unyanyasaji wa wanawake
kipindi chote cha uchaguzi.
Maazimio mengine ni kuwa Serikali za
nchi husika kuhakikisha kuwa kuna mtaala wa elimu kuhusu jinsia kadhalika
Serikali husika na wadau wengine kuhakikisha inatolewa elimu juu ya masuala ya
ushiriki wa wanawake katika uchaguzi.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment