Na
Innocent Natai, TPRI-Arusha
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega amesemakuwa
vita dhidi ya umaskini inahitajika kwenda sambamba na vita dhidi ya Gugu Karoti
kwani linamadahara kwa afya ya binadamu,mimea na wanyama hivyo kuleta umaskini
katika jamii hivyokurudihsha nyuma uchumi wa jamii.
Ameyasema hayo katika Mkutano wa wasiku ya gugu karoti
uliofanyika Jijini Arusha na kukutanisha wadau mbalimbali zikiwemo taasisi za
serikali na binafsi ikiwa na lengo la kutafuta namna ya kukabiliana na gugu
hilo ambalo linakuwa kwa kasi katika mkoa huo ili kujenga uelewa kwa jamii
Kwitega amesema wadau na wizara ya kilimo,mifugo, wataalam wa
afya ya binadamu na maliasili na utalii wanatakiwa kuunganisha nguvu
kuhakikisha wanatokomeza ikiwa ni kuona ueneaji na usambaaji wa visumbufu hivi
vamizi ili kuvitokomeza kwaajili ya kusaidia maisha ya binadamu wadudu na
wanyama.
Pia amewataka kamati ya kutokomeza gugu hili kujenga uelewa wa
kwa wadau wa kilimo,mifugo, wataalam wa afya ya binadamu na maliasili na
utaliiwa pia na mazingira ili kusaidia kuhamasisha jamii kushiriki kikamilifu
katika kupiga vita gugu hili.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa
Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical
Pesticides Research Institute-TPRI) Dr Esther Gwae Kimaro aliyewakilisha
Mkurugenzi Mkuu
Amesema kuwa taasisi hiyo kupitia kwa watafiti wamejitahidi
kuhakikisha wanakitokomeza kisumbufu hiki ikiwemo,kung’oa,na pia kwa kufanya
tafiti mbalimbali na kumsambaza mdudu katika mikoa mbalimbali ambapo gugu hili
limeonekana ukianzia na mkoani hapa Arusha ambae anakula gugu hili bila kuleta
madhara kwa viumbe wengine na mazingira.
Pia kutoa elimu kwa wadau mbalimbali ikiwemo katika maonyesho
mbalimbali mfano nanenane ili kuhakikisha wananchi wanalifahamu gugu hili na
madhara yake katika mazingira na kwa wanyama.9
Ramadhani
Kilewa ni Mtafiti kitengo cha kidhibiti visumbufu vya mimea
kutoka TPRI amesema kuwa Gugu karoti ni gugu hatari kwa wanyama na binadamu na
kwasasa limeenea baadhi ya mikoa hapa nchini Tanzania ikiwemo mkoa wa Arusha
hasa hasa katika maeneo mengi ya barabara na mashamba ya mazao.
Aidha amesemakuwa kamati ya kutokomeza Gugu karoti inakabiliwa
na changamoto ya rasilimali fedha ambapo ni tatizo kubwa kwani wakati wa
kiangazi kuung”oa huo mmea inahitajika kutumia vitendea kazi vya ziada na pia
usafiri kufika katika maeneo hayo.
‘’Tunaiomba serikali ya mkoa na wadau wengine kuungana nasi
katika kudhibiti gugu hili katika jamii kwa ujumla Ofisi yako itusaidie kama
tutapata hizo rasilimalifedha pia itusaidie kuwapa uelewa huu maafisa ugani,elimu
ndiyo pekee ndiyo inaweza kuleta usawa kwa jamii kwa kuwaeleza juu ya gugu
hili.’’ Alisema Kilewa
Jitihada
za ziada zinahitajika katika kupambana na na gugu hili kwani ni hatari
liliingia nchini haswa mkoa wa Arusha mwaka 2010 na linakuwa kwa kasi
mno,linapunguza kuota kwa mazao,ni hatari kwa afya ya binadamu na wanayama
,inahatarisha maisha ya viumbe wengine,linaweza kusababisha jangwa,inasababisha
pumu,na aleji ya ngozi kwa mujibu wa watafiti.
0 comments:
Post a Comment