Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Nishati wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua (hayupo pichani) kabla ya kuanza kazi ya uandaaji wa mikataba ya utendaji kazi katika utumishi wa umma kwa mwaka 2019/2020.
Baadhi ya Wataalam wa Wizara ya Nishati wakiwa katika kazi ya uandaaji wa mikataba ya utendaji kazi katika utumishi wa umma kwa mwaka 2019/2020.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua (katikati) akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Nishati kabla ya kuanza kazi ya uandaaji wa mikataba ya utendaji kazi katika utumishi wa umma kwa mwaka 2019/2020.
Na Teresia Mhagama
Wizara ya Nishati, imeanza kazi ya uandaaji wa mikataba ya utendaji kazi
katika utumishi wa umma kwa mwaka 2019/2020.
Kazi hiyo inayofanyika jijini Dodoma, imeratibiwa na Idara ya Sera na
Mipango katika Wizara ya Nishati ambapo uandaaji wa mikataba hiyo unafanyika
kwa uongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Akizungumza na Menejimenti ya Wizara ya Nishati kabla ya kuanza rasmi
kazi ya uandaaji wa mikataba hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi
Mwinyimvua, alisema kuwa, mikataba hiyo ni muhimu kwani katika kila
mwaka itapima kama watumishi wa umma wanatekeleza majukumu kadri ya malengo
yaliyowekwa kupitia Wizara, Taasisi, Idara au Kitengo.
Aliongeza kuwa, Watumishi wa Wizara ya Nishati, watakaohusika katika
uandaaji wa mikataba hiyo watapata uelewa zaidi kuhusu uandaaji wa malengo ya
Wizara, utekelezaji wake pamoja na upimaji wa malengo husika.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wizara ya Nishati, Haji
Janabi, alitoa wito kwa watumishi walioteuliwa kufanya kazi hiyo, kuhakikisha
kuwa wanaifanya kazi hiyo kwa ufanisi na kuikamilisha kwa wakati uliopangwa ili
ianze kutumika ndani ya muda uliopangwa na Serikali.
0 comments:
Post a Comment