METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, September 10, 2019

TANZANIA YAWEKEZEA MKAKATI WA KUTOKOMEZA UKATILI KWA WATOTO NA WANAWAKE

 Dr Naftari Ng’ondi kamishina wa ustawi wa jamii nchini Tanzania  amesema serikali ya Tanzania inaendelea kutekeleza
mkakati wa miaka mitano wa kutokomeza  ukatili wa kijinsia kwa wanawake na
watoto (Mtakua) ili kumaliza tatizo hilo ifikapo mwaka 2021.
 Baadhi ya wajumbe kutoka nchini Tanzania waliowakilisha mkutano wa msaada wa kisaikolojoa kwa watoto uliofanyika nchi Namibia
 Baadhi ya wajumbe kutoka nchini Tanzania waliowakilisha mkutano wa msaada wa kisaikolojoa kwa watoto uliofanyika nchi Namibia
 
Tumaini Godwin,Namibia.
 Serikali ya Tanzania inaendelea
kutekeleza mkakati wa miaka mitano wa kutokomeza  ukatili wa kijinsia kwa
wanawake na watoto (Mtakua) ili kumaliza tatizo hilo ifikapo mwaka 2021.
Kamishna wa Ustawi wa Jamii nchini
Tanzania, Dk Naftari Ng’ondi amesema hayo  wakati akiwasilisha mkakati huo
kwenye mkutano wa kimataifa wa msaada wa kisaikolojia kwa watoto(PSS FORUM)
unaofanyika Windhoek nchini Namibia.
Dk Ng’ondi amesema mkakati huo
ulioanza kutekelezwa tangu mwaka 2016  umetamka wazi kuwa pamoja na mambo yote,
tatizo la mimba na ndoa za utotoni linapaswa kushughulikiwa.
“Mimba za utotoni maana yake
kuna ubakaji umefanyika na  kwa Tanzania hilo ni kosa la jinai,
tumeimarisha sheria ya mtoto na yeyote anayekutwa na kosa la kumpa mimba
mwanafunzi anafungwa jela miaka 30,” amesema Kamishna huyo kutoka Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto.
Amesema mbali na sheria, wanatekeleza
mkakati huo kwa kuikarisha kamati za ulinzi wa mtoto kwenye kata kwa kuzipatia
nguvu ya kupokea, kuchunguza na kuchukua ikiwa ni pamoja na kufungua kesi.
Dk Ng’ondi amesema nguvu kubwa
imewekwa katika kutoka  elimu kwa Jamii na vijana kupitia kampeni
mbalimbali.
“Na sasa hivi tunaendesha
kampeni inayoitwa Twende pamoja, tokomeza ukatili,” amesema.
Awali Balozi wa Umoja wa Mataifa wa
Mpango wa kutokomeza mimba za utotoni, Nyaradzayi Gumbonzvanda alisema nchi za
Afrika zinapaswa kufanya kampeni ya kuhakikisha tatizo la mimba za utotoni
linaisha.
Amesema nchi nyingi za Afrika
zinakutana na changamoto ya mimba za utotoni huku umaskini ukichangia tatizo
hilo.
“Tuandae mkakati ya kumalizaa
tatizo,inawezekana,” amesema Gumbonzvanda.
Mkutano huo unaoendeshwa na Shirika
la Msaada wa Kisaikolojia kwa Watoto (REPPSI) umezikutanisha zaidi ya nchi 24
kutoka kusini mwa Afrika.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com