
Naibu Waziri wa
Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wafanyabiashara na wawekezaji wa
Mkoa wa Mtwara (hawapo pichani) katika Mkutano uliolenga kusikiliza
changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo Wafanyabiashara na Wawekezaji
mkoani Mtwara.

Baadhi ya
wafanyabiashara na wawekezaji wa Mkoa wa Mtwara wakiwa katika Mkutano
uliolenga kusikiliza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika
shughuli zao. Mkutano huo ulihusisha Mawaziri wanaosimamia Sekta
mbalimbali.

Baadhi ya
wafanyabiashara na wawekezaji wa Mkoa wa Mtwara wakiwa katika Mkutano
uliolenga kusikiliza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika
shughuli zao. Mkutano huo ulihusisha Mawaziri wanaosimamia Sekta
mbalimbali.

Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia akizungumza jambo katika
Mkutano uliolenga kusikiliza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo
Wafanyabiashara na Wawekezaji mkoani Mtwara. Mkutano huo ulihusisha
Mawaziri wanaosimamia Sekta mbalimbali.
……………………..
Na.Hafsa Omar,
Mtwara
Katika kuhakikisha kuwa Mkoa wa Mtwara
unakuwa na umeme wa uhakika kwa muda wote, Naibu waziri wa Nishati,
Subira Mgalu amewaeleza wafanyabishara na wawekezaji wa Mkoa huo kuwa,
Serikali ipo mbioni kujenga mitambo miwili mipya ya umeme.
Alisema hayo,
Septemba 25, 2019 wakati alipokuwa ajibu hoja za wadau wa maendeleo
katika mkutano uliolenga kusikiliza changamoto za wafanyabiashara na
wawekezaji wa Mkoa wa Mtwara, ambapo alisema Serikali inazifahamu
changamoto zote za umeme zinazojitokeza katika mkoa huo na tayari
zinafanyiwa kazi.
“Kituo cha
umeme cha Mtwara kina zaidi ya miaka 10 na baadhi ya mitambo imechakaa,
hapa ninavyozungumza sasa mitambo inayofanyakazi ni ile miwili tu mipya,
na mahitaji ya umeme katika mkoa wa Mtwara na Lindi yameongezeka,
kwani kwa sasa inatakiwa takriban megawati 17.7 wakati uwezo wa
uzalishaji katika Kituo cha Mtwara ni megawati 18 hivyo tunafanya
jitihada za kuongeza mitambo mipya.”Alisema Mgalu
Alifafanua,
Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), katika mwaka huu
wa fedha imetenga bajeti ya kununua mitambo miwili ambayo itasaidia
upatikanaji wa umeme wa uhakika.
Vile vile,
Naibu Waziri alisema hatua nyengine ambayo Serikali imechukua ni pamoja
kuwa na mpango wa muda mrefu utakaosaidia utapatikanaji wa umeme wa
uhakika mkoani humo.
“ Tunatarajia
kujenga mtambo wa kuzalisha umeme wa gesi hapa hapa Mtwara wa megawati
300 na njia ya kuusafirisha, pale Somangafungu pia kuna mpango wa
kujenga mtambo wa kuzalisha megawati 240 kwa kutumia gesi na njia ya
kuusafirisha kutoka Somangafungu hadi Kinyerezi, njia zote zitakuwa na
msongo wa kV 400 na tunategemea kutekeleza huu mradi kati ya mwaka
21/23.”alisema Mgalu
0 comments:
Post a Comment