Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Wasindikaji Wakubwa na wadogo wa korosho uliofanyika katika ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma tarehe 9 Septemba 2019. (Picha Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Wasindikaji Wakubwa na wadogo wa korosho uliofanyika katika ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma tarehe 9 Septemba 2019.
Sehemu ya wabanguaji wa korosho wakifatilia mkutano wa waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) wakati wakati akizungumza kwenye mkutano wake na Wasindikaji Wakubwa na wadogo wa korosho uliofanyika katika ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma tarehe 9 Septemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Wasindikaji Wakubwa na wadogo wa korosho uliofanyika katika ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma tarehe 9 Septemba 2019.
Na Issa Sabuni, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Waziri
wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) amewaambia Wasindikaji wadogo na Wakubwa wa
korosho kuwa lengo la Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Mhe Dtk
John Pombe Magufuli ni kuongeza kiwango kikubwa cha usindikaji kuliko ilivyokuwa
mwaka jana na kwamba Serikali haitanunua tena korosho bali itaweka mazingira
mazuri kwa Wafanyabiashara kununua zao hilo kutoka kwa Wakulima bila ya
kuwalalia.
Mhe
Hasunga ameyasema hayo katika mkutano wake maaalum alioutisha tarehe 9 Septemba
2019 katika ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma lengo likiwa ni kuzungumza
na Wasindikaji hao ili kujiandaa na msimu mpya wa ununuzi wa korosho ambapo
taarifa rasmi ya Wizara itatolewa hivi karibuni.
Waziri
Hasunga amesema licha ya Serikali kuendelea na azma yake ya kuongeza thamani ya
zao la korosho kwa kuwasisitiza Wabanguaji kuongeza ubora na uwezo wa korosho
watakazobangua zaidi ya ilivyokuwa msimu uliopita.
“Tumeona
kabla ya kutangaza taarifa rasmi ya Wizara yenye kuzindua rasmi msimu mpya wa
ununuzi wa korosho, ni vyema tukutane nanyi Wadau ili kujadiliana namna nzuri
ya kuboresha biashara ya korosho kwa lengo la manufaa ya Wakulima wetu”
Amekaririwa Waziri Hasunga
Katika
hotuba yake; Waziri Hasunga ameelekeza kuwa Wabanguaji hao wanapaswa kutoa
Taarifa kwa Wizara kwa msimu wa kilimo wa 2019/2020 katika maeneo kadhaa
ikiwemo teknolojia wanazotumia katika ubanguaji na usindikaji wa korosho, uwezo
wa mashine zao kusindika kwa mwaka, idadi ya Wafanyakazi walioajiriwa katika viwanda,
uwezo wa viwanda kubangua na kusindika korosho kwa mwezi na kwa mwaka vilevile mapendekezo
ya bei ya kununulia kabla ya msimu kuanza.
Waziri
Hasunga ameongeza kuwa Wasindikaji pia wanapaswa kuwa wa wazi katika kuishauri
Serikali namna nzuri ya kuboresha zoezi zima la ununuzi mpya wa korosho na
kueleza changamoto wanazokutana nazo.
Awali
katika taarifa yake, Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Bwana Francis Alfred
amesema uzalishaji wa korosho kwa msimu huu unataraji kufikia tani laki 3 na
nusu (350,000) na kuongeza kuwa tija itaongezeka ikiwa sehemu kubwa ya
uzalishaji itabanguliwa na kusindikwa hapa hapa nchini.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment