Baadhi
ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba wakiwa katika eneo la ujenzi wa
Soko la Mazao la Kakozi wakijadiliana namna ya kuharakisha ujenzi huo ambapo
mpaka sasa serikali imeshatoa shilingi bilioni mbili.
Vibarua
wakiendelea na ujenzi wa Soko la Mazao la Kakozi ambapo mpaka sasa serikali
imeshatoa shilingi bilioni mbili.
...................
Uwepo
wa makundi yasiyo na tija, kutegeana katika kazi na kutoshirikiana baina ya
watumishi kumesababisha miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika halmashauri ya
Wilaya ya Momba kuchelewa kukamilika.
Hayo
yamebainishwa jana na baadhi ya watumishi wa Halmashauri hiyo walipokuwa
wakizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela
alipokutana nao kutaka kufahamu sababu za kutokamilika kwa wakati ujenzi wa
miradi mbalimbali katika halmashauri hiyo.
Mmoja
wa watumishi amesema, “unapokuwa na mradi wa sekta fulani mfano afya, kilimo au
elimu watumishi wenzako wanakaa pembeni hawakusaidii, ni kama wanakutegea waone
utakavyoshindwa kitu ambacho sio sahihi, miradi yote ni ya halmashauri na
inalenga kuwanufaisha wananchi wote.”
Watumishi
hao wamesema baada ya kuzungumza na Mkuu wa Mkoa wameona kuwa makundi na
kutoshirikiana havitaijenga halmashauri na hivyo wameapa kubadilika na kufanya
kazi kwa pamoja kama timu moja.
Aidha
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela amesema anaamini tatizo la
kutoshirikiana baina ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba limeisha na
watafanya kazi kwa pamoja.
Brig.
Jen. Mwangela ameongeza kuwa mara baada ya kikao hicho ameona ushirikiano wa
watumishi katika ujenzi wa Soko la Mazao la Kakozi ambapo wote kwa pamoja
wameonyesha nia kufanikisha ujenzi huo kwakuwa umesha chelewa kwa zaidi ya
miezi sita.
Naye
Msimamizi wa Ujenzi wa soko la mazao la Kakozi Aloyce Sakaya amesema kwa sasa
mradi huo utatekelezwa kwa kasi zaidi kwakuwa changamoto zilizo sababisha ukachelewa
ikiwa ni pamoja na kutoshirikiana baina yao zimeondolewa.
0 comments:
Post a Comment