
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe.
Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza na wananchi wa wa Kijiji cha Kalamba
wilayani Kondoa, ambapo wananchi hao
walimuomba awahimize Watendaji wake ili jengo la Kituo cha Afya Kalamba
likamilike na kuanza kutoa huduma kwa Wanakijiji hao.

Baadhi ya
Wananchi wa Kijiji cha Kalamba wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu
Kijaji (hayupo pichani), alipokuwa akitoa maelekezo kwa Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Bw. Mashauri Vicent
(hayupo pichani) kuhusu umaliziaji wa Kituo cha Afya cha Kalamba ambacho
kitakuwa kikihudumia zaidi ya Wanakijiji 13,000 wa Kalamba na Haubi.

Dkt. Alpha
Kwilasa wa Kituo cha Afya cha Busi akimueleza Naibu Waziri wa Fedha na
Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji
huduma zinazotolewa katika kituo hicho cha afya wilayani Kondoa.

Kaimu
Mhandisi wa Wilaya Bw. Felchism Tesha akimuonesha bajeti ya matumizi ya
fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Kituo
cha Afya Kalamba Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge
wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji alipotembelea Miradi ya
Ujenzi wa Vituo cha Afya Wilayani humo.

Jengo la Maabara katika Kituo cha Afya Busi linalotoa huduma kwa Wanakijiji wa Kijiji hicho wilayani Kondoa.

Naibu Waziri
wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt.
Ashatu Kijaji akikagua chumba cha kuhifadhia maiti alipotembelea miradi
ya Ujenzi wa Vituo cha Afya Wilayani humo.

Naibu Waziri
wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt.
Ashatu Kijaji akitoa maagizo kwa uongozi wa kijiji hukakikisha
wanafuatilia kila hatua ya utekelezaji wa miradi inayotekelezwa katika
vijiji vyao ili viweze kumalizika kwa wakati alipotembelea wilayani
humo.
…………………
Na Josephine Majura, Kondoa
Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ametoa muda wa siku 37 kwa
uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kuhakikisha kuwa ujenzi wa
vituo vitatu vya afya vya Bereko, Thawi na Kalamba vinakamilika na
kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Dkt. Kijaji
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini, ametoa maagizo hayo
alipofanya ziara ya kutembelea mradi ya ujenzi wa vituo vya afya
vinavyojengwa kwa fedha za Serikali katika vijiji mbalimbali Wilayani
Kondoa, mkoani Dodoma, ambapo alibaini kuna uzembe katika umaliziaji wa
ujenzi wa baadhi ya vituo hivyo kikiwemo Kituo cha Afya Kalamba.
Alielezea
kutoridhika na utendajikazi wa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo
katika usimamizi wa miradi hiyo muhimu kwa wananchi wakati Serikali
ilikwishatoa fedha zote za kukamilisha miradi hiyo na kuagiza hadi
Oktoba 30 mwaka huu miradi hiyo iwe imekamilika.
“Dhamira njema
ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Mhe. Dkt. John Joseph Pombe
Magufuli yakuleta milioni 400 kwenye kituo hichi cha Afya ni kupata
huduma lakini hatujaanza kutoa huduma hiyo kwa zaidi ya mwaka sasa”,
alisema Dkt. Kijaji.
Aliiagiza
Ofisi ya Mkoa na Wilaya hukakikisha wanafuatilia vizuri utekelezaji wa
miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi inayofadhiliwa na Serikali
ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati kwa sababu Serikali haianzishi
mradi mpya bila kutoa fedha zote za miradi husika.
Serikali ilitoa
fedha kwa nyakati tofauti kwa ajili ya mradi wa Ujenzi wa vituo vya
afya vitano wilayani Kondoa kati ya vituo hivyo, vituo viwili vya Mauno
na Busi vimekamilika, huku vituo vitatu vya afya vya Bereko, Thawi na
Kalamba havijakamilika.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kondoa Bw. Mashauri Vicent alimuahidi Dkt. Kijaji kutekeleza magizo yote aliyoyatoa hasa ya kulipwa kwa watumishi waliofanya kazi mbalimbali kwenye vituo hivyo vya afya ndani ya siku 14.
Naye
Mwanakijiji wa Mauno Bw. Haji Selemani, ameishukuru Serikali kwa juhudi
mbalimbali inayofanya katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo
hasa huduma za jamii na kusifia huduma inayotolewa na Watumishi wa Kituo
cha Afya Busi.
Kwa upande wake Mwanakijiji cha Bereko Bw. Juma Saidi amempongeza Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe.
Dkt. Ashatu Kijaji kwa kazi kubwa anayoifanya jimboni huko na kumuombea
afya njema ili awe na nguvu yakufanya kazi na zaidi.
0 comments:
Post a Comment