Watumishi
wa Afya wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa, Bukoba, mkoani
Kagera,wakiendelea kufanya mazoezi ya namna ya kumhudumia mgonjwa
anayehisiwa kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa Ebola, katika hospitali
hiyo Agosti 2019.
Mratibu wa zoezi hilo toka Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, ambaye pia ni
Mtaalamu wa Afya ya Jamii, Dharura na Maafa, Dkt. Faraja akiendelea na
shughuli za uwezeshaji wa zoezi la kupima utayari wa kukabili wa ugonjwa
wa Ebola kwa watumishi wa Afya wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa, Bukoba,
mkoani Kagera, Agosti 2019.
Watumishi wa Afya wa Hospitali ya
Rufaa ya mkoa, Bukoba, mkoani Kagera,wakiendelea kufanya mazoezi ya
namna ya kuvaa vifaa kinga kwa ajili ya kumhudumia mgonjwa anayehisiwa
kuwa na maabukizi ya ugonjwa wa Ebola, katika hospitali hiyo Agosti
2019.
Afya wa Afya katika Kituo cha Afya
Bunazi mkoani Kagera,akiendelea kufanya mazoezi ya namna ya kumhudumia
mgonjwa anayehisiwa kuwa na maabukizi ya ugonjwa wa Ebola, katika
hospitali hiyo Agosti 2019.
Waratibu
wa zoezi la kupima Utayari wa kukabili mlipuko wa ugonjwa wa Ebola
kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto,
wakiendelea kufafanua utekelezaji wa zoezi hilo kwa mtumishi wa Afya
katika kituo cha Afya cha Bunazi, mkoani Kagera Agosti 2019.
Watumishi wa Afya wa Hospitali ya
Rufaa ya mkoa, Bukoba, mkoani Kagera,wakiendelea kufanya mazoezi ya
namna ya kuvaa vifaa kinga kwa ajili ya kumhudumia mgonjwa anayehisiwa
kuwa na maabukizi ya ugonjwa wa Ebola, katika hospitali hiyo Agosti
2019.
Waratibu wa zoezi la kupima
Utayari wa kukabili mlipuko wa ugonjwa wa Ebola, wakiendelea kuelekeza
namna ya kuvaa vifaa kinga kwa watumishi wa Afya katika kituo cha Afya
cha Bunazi, mkoani Kagera Agosti 2019.
******
Na. OWM, KAGERA
Serikali kupitia uratibu wa Ofisi
ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa kwa kushirikiana na Wizara
ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, pamoja na wadau wa
maendeleo, imefanikiwa kufanya zoezi la kupima utayari wa kukabili
ugonjwa wa Ebola katika mkoa wa Kagera katika wilaya tatu za mkoa huo
kwa kuhusisha watoa huduma za Afya katika wilaya hizo za Bukoba,
Misenyi na Ngara.
Zoezi hilo limefanikiwa
kuwaimarisha watumishi hao katika maeneo maalum ikiwemo ya uratibu,
utambuzi na ufuatiliaji wa wagonjwa iwapo wakipatina, matibabu ya
wagonjwa, uchukuaji na usafirishaji wa sampuli na kuthibitisha maabukizi
pamoja kuimarisha mifumo ya utambuzi wa masuala ya Afya kwa kila abiria
wanaopita kwenye mipaka ya mkoa wa Kagera.
Akiongea kuhusu kuhitimishwa kwa
zoezi hilo jana tarehe 3 Agosti, 2019, mkoani Kagera, Mkurugenzi
Msaidizi (Utafiti na Mipango), Idara ya Menejimenti ya Maafa, ofisi ya
Waziri Mkuu, Bashiru Taratibu, ameeleza kuwa watumishi wa sekta ya Afya
katika maeneo yote ambayo zoezi hilo limefanyika wameweza kuimarishwa
katika suala la uratibu hususani katika kuhakikisha kuwa rasilimali
zote zinazohitajika pindi ikigundulika kuwepo kwa mgonjwa wa Ebola
zinapatikana kwa wakati na kwa kutosheleza mahitaji pamoja na kutumika
kwa usahihi.
Aidha, Mratibu wa zoezi hilo toka
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, ambaye pia
ni Mtaalamu wa Afya ya Jamii, Dharura na Maafa, Dkt. Faraja Msemwa
amefafanua kuwa timu ya wataalamu wa sekta za Afya na Uratibu wa
Shughuli za serikali, kutoka Wizarani, Idara na Mashirika ya
Kimataifa, wamefanikiwa kuendesha zoezi hilo kwa watoa huduma wa
Afya kwa wilaya tatu za mkoa huo hususan zilizopo mipakani.
“Zoezi letu tumefanikiwa
kulihitimisha mkoani hapa tayari kwa kufanya zoezi la kupima utayari wa
kukabili ugonjwa wa Ebola kwa watoa huduma wa Afya kwa vituo vya Afya
vya Nshambya, Kabyaile, Kabanga, Bunazi pamoja na Hospitali ya Rufaa ya
mkoa ya Bukoba.Tunaamini kufanikiwa kufanya zoezi hili limeboresha
utendeji wa watoa huduma hao katika kukabili ugonjwa wa Ebloa” alisema
Dkt. Msemwa
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa
Mkoa huo, Dkt. Marco Mbata amefafanua kuwa kufanyika kwa zoezi hilo
mkoani humo kumewawezesha kujua maeneo gani ya kuboresha wakati wa
ugonjwa wa Ebola na watumishi wameelewa kwa vitendo wapo tayari
kukabili ugonjwa huo.
“Tunashukuru vifaa tunavyo vya
kutumia wakati wa kujikinga iwapo atatokea mgonjwa wa Ebola, hivyo
kupitia zoezi hili tumeongeza uelewa wa kujikinga wenyewe, kuwakiknga
watu walio karibu na mgonjwa pamoja na jamii nzima. Tumeweza kujifunza
jinsi ya kumpokea mgonjwa, kuchukua vipimo hakika zoezi hili limetujenga
” alisisitiza Mbata.
Naye Mratibu wa Vituo vya
Mipakani, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto,
Remedius Kakuru amebainisha kuwa kupitia zoezi hilo limeimarisha
utendaji wa maafisa Afya wa mipakani kwa kuzingatia kuwa tayari
serikali imenunua vifaa vya kisasa muhimu vinavyo hitajika kwa ajili ya
utambuzi wa abiria mwenye maambukizi ya ugonjwa wa Ebola ikiwemo Vipima
joto la mwili “themo scanners”.Vifaa hivyo vyenye uwezo wa kupima joto
la mwili la abiria wanao pita katika mipaka ya Tanzania vina uwezo wa
kupima joto la mwili kwa kuwa ndiyo kiashiria kikuu kimojawapo kwa
mgonjwa mwenye maabukizi ya Ebola .
Kwa upande wake Afisa
anayeshughulika na Magonjwa ya Mlipuko kutoka Shirika la Afya Duniani,
hapa nchini, Anthony Kazoka alieleza kuwa Shirika la Afya Duniani
linaendelea kushirikiana na serikalai ya Tanzania katika kulinda Afya za
watu wake kwa kutoa utaalamu katika zoezi hilo kwa kuwa Tanzania ni
miongoni mwa nchi ambazo zimo hatarini kupata mlipuko wa ugonjwa wa
Ebola. Hivyo kwa kufanyika zoezi hilo kwa mafanikio kutasaidia Tanzania
kuwa salama na kuwa chanzo cha kuiweka Dunia salama kwa kutambua
maabukizi ya ugonjwa huo mapema iwapo yatatokea.
Kufuatia nchi ya jirani (DRC)
kuendelea kukabiliwa na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola tangu Agosti mwaka
2018. Tanzania imeendelea kuchukua tahadhari za ugonjwa huo kwa kupima
utayari wa Watoa huduma za Afya kwa mikoa ya mipakani ukiwemo mkoa wa
Kagera. Mkoa huo ambao unapakana na nchi ya Uganda ambayo inapakana na
DRC lakini pia imekuwa na wagonjwa kadhaa wa Ebola.
Zoezi hilo linaratibiwa na Ofisi
ya Waziri Mkuu na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto kwa ushirikiano na wadau wa maendeleo ambao ni WHO, FAO, USAID,
HRH2030, na USAID Global Health Supply Chain Programu. Zoezi hilo
limefanyika kwa muda wa wiki moja ambapo limekamilika tarehe 3 Agosti
mwaka 2019, kwa kufanyika katika vituo vya kutolea huduma za afya na
maeneo ya mipaka ya mkoani wa Kagera.
0 comments:
Post a Comment