





Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe. George
Boniface Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na wananchi
wanaosimamia mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Kianga pamoja na watendaji
kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wa Muungano na Makamu wa Pili wa Zanzibar.
*************
Na Ofisi ya Makamu wa Rais
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. George
Boniface Simbachawene ameupongeza mradi wa utunzaji mazingira kupitia
upandaji miti ya mikoko mjini Zanzibar.
Mhe. Simbachawene ametoa pongezi hizo Agosti 5, 2019 katika siku ya kwanza
ya ziara yake ya kujitambulisha na kukagua miradi ya Muungano na Mazingira
visiwani hapa.
Akiwa katika eneo hilo lenye hekta nne lililopo Shehia ya Kilimani Wilaya ya Mjini
Mkoa wa Magharibi alisema ameridhishwa kuona namna ambavyo Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ilivyotekeleza mradi huo pamoja na ufadhili
kutoka Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP).
“Niwapongeze sana kwa mradi huu mzuri na tunaona matokeo yake umesaidia
mawimbi yasije kwa kasi katika eneo hili na kusababisha mmonyoko na tukiamua
kufanya kazi kwa pamonja na jamii tunaweza kufanya vizuri,” alisema.
Aidha, Mhe. Simbachawene alitoa wito kwa wataalamu kuangalia namna ya
kuibua miradi mingine katika fukwe za mikoa mingine kama Dar es Salaam,
Tanga, Lindi na Mtwara ili kusaidia kutunza mazingira.
Katika hatua nyingine alikagua ujenzi wa Kituo cha Afya Kianga katika Wilaya ya
Magharibi A Mkoa wa Mjini Magharibi aliwapongeza wananchi kwa kusimamia
mradi huo.
Alisema kuwa kwa kiasi cha sh. milioni 174 inadhihrisha namna wanavyotumia
fedha kwa uaminifu na kuwa tutapiga hatua katika kuendeleza sekta ya huduma
ya afya kwa wananchi.
“Nawapongeza sana wananchi hasa kwa kamati hii mmefanya vizuri kusimamia
mradi huu wa ujenzi wa kituo cha afya tunaamini udokozi haukuwepo kazi
imefanyika fenicha (samani) zipo, vifaa tiba na utendaji kazi mzuri unaendelea
kufanyika,” alisema.
0 comments:
Post a Comment