NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta, timu yake, KRC Genk ya
Ubelgiji imepangwa kundi moja na E Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na
mabingwa watetezi, Liverpool ya England, Napoli ya Italia na Salzburg ya
Austria.
Katika droo ya michuano hiyo iliyofanyika sambamba na tuzo za
Mwanasoka Bora Ulaya, Samatta amejikuta akinagushiwa kwenye kundi la
mabingwa watetezi, Liverpool na maana yake atakutana tena na Sadio Mane
wa Senegal.
Mane aliiongoza Senegal kuichapa Tanzania ya Samatta 2-0 kwenye
mechi ya Kundi C Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Juni mwaka huu
nchini Misri. Huko walikuwa na Mohamed Salah wa Liverpool, ambaye timu
yake, Misri kama Tanzania ilitolewa mapema.
Simba wa Teranga walifanikiwa kwenda hadi fainali, ambako
walikutana tena na wapinzani wao wa Kundi A, Algeria na kuchapwa tena
1-0, bao pekee la Baghdad Bounedjah dakika ya pili tu Uwanja wa
Kimataifa wa Cairo hivyo kulikosa taji la AFCON.
Kundi A linaundwa na PSG ya Ufaransa, Real Madrid ya Hispania,
Club Brugge ya Ubelgiji na Galatasaray ya Uturuki, Kundi kuna Bayern
Munich ya Ujerumani, Tottenham Hotspur ya England, Olympiacos ya Ugiriki
na Red Star Belgrade ya Serbia.
Kundi C linaundwa na Manchester City ya England, Shakhtar
Donetsk ya Ukraine, GNK Dinamo ya Croatia na Atalanta ya Italia, Kundi D
linaundwa na Juventus ya Italia, Atletico Madrid ya Hispania, Bayer
Leverkusen ya Ujerumani na Lokomotiv Moskow ya Urusi.
Kundi E ndio Liverpool, Napoli, Salzburg na KRC Genk, Kundi F
kuna Barcelona ya Hispania, Borussia Dortmund ya Ujerumani, Inter Milan
ya Italia na Slavia Praha Jamhuri ya Czech, Kundi G lina Zenit ya Urusi,
Benfica ya Ureno, Lyon ya Ufaransa na RB Leipzig ya Ujerumani na Kundi H
linazikutanisha Chelsea ya England, Ajax ya Uholanzi, Valencia ya
Hispania na Lille ya Ufaransa.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Samatta kucheza Ligi ya Mabingwa
Ulaya baada ya kuisaidia Genk kutwaa ubingwa wa Ubelgiji msimu uliopita.
Lakini msimu uliopita alicheza michuano ya Europa League na timu
yake, Genk ilitolewa hatua ya 32 Bora Slavia Prague ya Czech kwa
kuchapwa 4-1 nyumbani baada ya sare ya 0-0 ugenini.
Thursday, August 29, 2019
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
📌 Asema Rais, Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Watanzaia 📌 Atak...
-
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI, Dkt. Respicious Boniface akizungumza na Waandishi wa Habari (ha...
-
Mvua kubwa za El-Nino zilizonyesha zimeleta athari maeneo mbalimbali...
-
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza katika Uzinduzi wa Siku 16 za kupinga Ukatili d...
-
Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga akikagua ghala la kuhifadhia mbegu la Wakala wa Mbegu (ASA) katika ziara yake ya kikazi mkoani Morogo...
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment