NA EVELINA ODEMBA-OFISI YA DED SIKONGE
WATU
wawili raia wa Afrika Kusini wafariki katika ajali ya ndege iliyotokea
mapema asubuhi ya leo majira ya saa moja na nusu katika kata ya Igigwa
Wilayani Sikonge.
Watu
hao waliotambulika kwa majina ya D. Werner mwenye umri wa miaka hamsini
na nane 58 pamoja na Werner Fredrick Fronaman mwenye umri wa miaka 36
wote wanamme na raia wa Durbun Afrika ya kusini walikuwa kwenye ndege
yenye namba za usajili 19-ZU-TAF mali ya Afrika Kusini.
Akilezea
tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Peres Magiri alisema kuwa
amepokea kwa masikitiko makubwa tukio hilo na kusema kuwa watu hao ambao
walikuwa katika ziara ya kuhamasisha wanafunzi barani Afrika kusomea
maswala ya Anga.
Kabla
ya ajari kutokea hapo jana walitua kwa dharula katika uwanja wa ndege
wa Tabora wakitokea Entebe Uganda kuelekea Lilongwe Malawi ili kufika
Afrika ya kusini. Ambapo asubuhi ya leo walipoanza safari baada ya muda
mchache walifanya mawasiliano na wataalamu wa uwanja wa ndege wa Tabora
na kutoa taarifa kuwa injini ya ndege imezimika ghafla wakiwa angani
hivyo wanafanya utaratibu wa kurudi Tabora baada ya taarifa hizo
hawakuweza kupatikana mpaka walipopata taarifa ya ajali hiyo na kufika
wakakuta raia hao wameshafariki.
0 comments:
Post a Comment