Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii, Ruth Minja akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari wakati alipokuwa akitoa taarifa ya mfumuko wa bei kwa kipindi cha mwaka ulioishia mwezi Julai 2019. Kulia ni Kaimu Meneja wa Takwimu za Ajira na Bei, Gregory Millinga. Mkutano huo ulifanyika leo Ijumaa Agosti 9, 2019.
Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii, Ruth Minja akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari wakati alipokuwa akitoa taarifa ya mfumuko wa bei kwa kipindi cha mwaka ulioishia mwezi Julai 2019.
(PICHA NA MAELEZO).
****************
Na Mwandishi Wetu,
MAELEZO
DAR ES SALAAM
Ofisi ya Taifa ya Takwimu imetoa
taarifa ya mfumuko wa bei nchini ambapo pamoja na mambo mengine mfumuko
wa bei ya mwezi Julai 2019, umebakia kuwa asilimia 3.7 kama ilivyokuwa
kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2019.
Akizungumza na waandishi wa vyombo
vya habari leo Ijumaa (Agosti 9, 2019) Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya
Watu na Takwimu za Jamii, Ruth Minja alisema kiwango hichi kubakia kuwa
sawa kwa kiwango hicho kumechangiwa na kuongezeka na kupungua kwa bei za
baadhi za vyakula na bidhaa zisizo za chakula kwa kipindi kilichoisha
Julai 2019.
Aidha Minja alisema mfumuko wa bei
wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Julai 2019
umeongezeka kidogo hadi kufikia asilimia 2.9 kutoka asilimia 2.3
ilivyokuwa kwa mwezi Juni 2019.
“Baadhi ya bidhaa zilizoongezeka
bei kwa mwezi Julai zikilinganishwa na Julai 2018 ni pamoja na unga wa
mahindi (6.0%), unga wa mhogo (4.0%), mafuta ya kupikia (8.9%), na
mbogamboga (4.6%) ambapo kwa uoande wa bidhaa zisizokuwa za vyakula ni
pamoja na vifaa vya kieletroniki, majiko ya gesi pamoja na vifaa pamoja
na bidhaa za huduma”.
Akizungumzia hali ya mfumuko wa
bei kwa baadhi ya Nchi za Afrika Mashariki, taarifa inaonyesha kuwa Nchi
ya Kenya ilikuwa na Kiwango cha juu cha mfumuko wa bei kwa mwezi Julai
2019, ambapo kiwango chake kilifikia asilimia 6.27 ikilinganishwa na
asilimia 5.70 kwa mwaka ulioishia Juni 2019.
Akifafanaua zaidi Minja alisema
taarifa ya mfumuko wa bei katika Nchi ya Uganda katika mwaka ulioishia
Julai 2019, taarifa zinaonyesha kuwa Nchi hiyo ilikuwa na kiwango kidogo
cha mfumuko wa mdogo bei kilichofikia asilimia 2.6 kutoka asilimia 3.4
kwa mwaka ulioishia Juni, 2019.
0 comments:
Post a Comment