Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akimpa pole Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi
wakati alipoiwakilisha serikali katika mazishi ya Mke wa mwanasheria
Mkuu wa Serikali, Natalia Bahati Kilangi yaliyofanyika Luchelele jijini
Mwanza, Agosti 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
akizungumza katika mazishi ya Natalia Bahati Kilangi, Mke wa Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi yaliyofanyika Luchelele
jijini Mwanza, Agosti 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
Spika wa Bunge, Job Ndugai (kulia kwa Waziri Mkuu) wakishiriki katika
ibada ya mazishi ya Natalia Bahati Kilangi, Mke wa Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Profesa Adelardus Kilangi yaliyoanyika Luchelele jijini
Mwanza, Agosti 7, 2019. Wengine pichani kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa
CCM, Dkt. Bashiru Ally, Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Augustine
Mahiga, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,
Vijana,Ajira, na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kulia ni Waziri wa
Madini, Doto Biteko. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akitoa heshima za mwisho kwa Natalia Bahati Kilangi, Mke wa Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi katika mazishi yaliyofanyika
Luchelele jijini Mwanza, Agosti 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akitupa udongo kwenye kaburi la Natalia Bahati Kilangi, Mke wa
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi, katika mazishi
yaliyofanyika Luchelele jijini Mwanza, Agosti 7, 2019. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Serikali, Profesa Adelardus Kilangi (wa pili kushoto) na familia yake
wakishiriki katika Ibada ya mazishi ya Natalia Bahati Kilangi, Mke wa
Mwanasheria Mkuu wa Serikali yaliyofanyika Luchelele jijini Mwanaza
Agosti 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiweka shada la maua kwenye kaburi la Natalia Bahati Kilangi, Mke wa
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi katika mazishi
yaliyofanyika nyumbani kwa Profesa Kilangi, Luchelele jijini Mwanza,
Agosti 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuui, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza, Renatus Nkwande na
Askofu wa Jimbo la Geita, Flavian Kassala katika mazishi ya Natalia
Bahati Kilangi, Mke wa mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus
Kilangi yaliyofanyika Luchelele jijini Mwanza, Agosti 7, 2019. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
*************
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo,
Agosti 7, 2019 ameongoza mazishi ya mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali,
Profesa Adelardus Kilangi, Bibi Natalia Bahati Kilangi.
Akizungumza kwa niaba ya
Serikali katika mazishi hayo yaliyofanyika nyumbani kwa Profesa Kilangi
eneo la Luchelele jijini Mwanza, Waziri Mkuu amemuomba Profesa Kilangi
na familia yake kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu ambapo
wamempoteza mama ambaye ni nguzo muhimu ya familia.
Kadhalika, Waziri Mkuu
ametumia fursa hiyo kuwasilisha salamu za pole kutoka kwa Rais Dkt. John
Magufuli kwa Profesa Kilangi na familia yake kutokana na msiba mzito
walioupata.
Katika salamu zake Rais Dkt.
Magufuli amesema Serikali inathamini sana mchango mkubwa na mahili
unaotolewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na anamini kwamba kwa
vyovyote vile wakati wa uhai wake, marehemu Natalia alishiriki kwa
kiwango kikubwa kuhakikisha kwamba mumewe anaifanya kazi yake vizuri.
Awali, Spika wa Bunge, Job
Ndugai aliwasihi waombolezaji wote wamkumbuke katika sala zao,
Mwanasheria Mkuu wa Seriakali Profesa Kilangi ambaye ana kazi nzito ya
kuishauri Serikali na alimtaja kuwa ni kiungo muhimu cha mihimili yote
mitatu.
Naye, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu
Katoliki la Mwanza, Renatus Nkwande alimuomba Profesa Kilangi na
familia yake wajipe moyo kwa sababu binadamu anapokuwa hai au anapokufa
bado anabaki kuwa mali ya Mwenyezi Mungu.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa
Umoja wa Wamiliki wa Mabenki nchini, Abdulmajid Msekela ambaye pia ni
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB alisema wanachama wote wa umoja huo wanatoa
pole kwa familia na wanamwombea Mwanasheria Mkuu wa Serikali na familia
nzima, Mungu awape uvumilivu katika kipindi hiki cha majonzi.
Baadhi ya viongozi
waliohudhuria katika mazishi hayo ni pamoja na Waziri wa Katiba na
Sheria, Balozi Augustine Mahiga, Waziri wa Madini, Doto Biteko, Waziri
wa Kilimo, Japhet Hasunga.
Wengine ni Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,
Jenista Mhagama na Katibu Mkuu wa CCM, Bashiru Ally, Manaibu
Mawazi, Wakuu wa Mikoa na wilaya na viomgozi mbalimbali wa Serikali.
Mazishi hayo pia yalihudhuriwa
na Askofu wa Jimbo la Geita na Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu
Katoliki Tanzania(TEC), Flavian Kassala, Mapadri na Masheikh kutoka
maeneo mbalimbali nchini
0 comments:
Post a Comment