METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, August 7, 2019

ALIYOYASEMA KATIBU WA CCM MKOA WA MOROGORO WAKATI AKITOA SALAMU ZA CCM KWA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE SAMIA S.HASSAN KATIKA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI KIWANDA CHA KUMENYA MPUNGA JUMATANO 07/08/2019 KIHONDA VIWANDANI



"Mhe Makamu wa Rais sisi viongozi wenzenu kwa kufata matakwa ya katiba ya CCM tumejiwekea utaratibu wa kushuka kwa wananchi kuwaelezea mafanikio ya ilani ya CCM" Shaka

"Na mnapokuja ninyi viongozi wetu wa kitaifa sisi ni wajibu wetu kuwatia moyo na ari ili muendelee kufanya kazi  vizuri zaidi" Shaka

"Rais wa kwanza Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere alipokuwa mstari wa mbele kupigania uhuru na baadae  ukombozi kusini mwa Afrika hakufahamika lakini baada ya ukombozi kukamilika anaendelea kusifiwa na heshima hiyo ni urithi kwa watanzania wote leo" Shaka

"Wakati Mwalimu Nyerere alipokuwa akienda huku na huko kuweka mipango ya ukombozi pamoja na wenzake, wapo waliomponda lakini baada ya kujikomboa  imekuwa ni sifa ya pamoja ya watanzania wote" Shaka

"Upo msemo wa wahenga nabii hakubaliki kwao,  ila kwa Magufuli imekuwa tofauti Magufuli anakubalika kwao, Afrika na Duniani kwa ujumla kutokana na mipango madhubuti, uwajibikaji uzalendo na utayari wa kulitumikia  Taifa" Shaka

"Heshima ya Tanzania ni kubwa mbele ya macho ya dunia na afrika kwa ujumla mhe makamu wa Rais endeleeni kuchapa kazi walio wengi kama si wote tunawaelewa  nia na nadhamira yenu kwa watanzania kupitia ilani ya CCM" Shaka

"Yote yanayofanyika sasa ni mazuri na ya kimaendeleo, wapo watu hawana uungwana na utamaduni wa kumsifu mtu akiwa hai. Wanaona kama wakimsifu watakuwa wamejikashifu. Aina hiyo ni ya watu wachoyo na wanafiki ambao hawakosekani katika Kila jamii " Shaka

"Hata yanayofanywa sasa chini ya serikali ya awamu ya tano kwa wakati huu wapo watakaoyabeza bila aibu lakini mwishowe wabezaji ndiyo watakuwa washangiliaji" Shaka

"Hatupati dhambi kwa kusifu mema na mazuri ya kimaendeleo yanayofanywa na Dk Magufuli katika utawala wake. Tukimsifu ndipo tutakapompa nguvu ya kutenda zaidi kwa manufaa ya Taifa " Shak
a
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com