METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, July 19, 2019

Ziara ya Naibu Waziri Subira Mgalu Ukaguzi Miradi ya REA Mkoani Kigoma

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akionyesha kifaa maalum cha kuunganishia umeme kwenye nyumba ambazo hazijawekewa mfumo wa kusambazia umeme kijulikanacho kama Umeme Tayari (UMETA) wakati wa mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nyange wilayani Kibondo mkoa wa Kigoma hivi karibuni. Naibu Waziri Mgalu alikuwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya usambazaji wa umeme vijini inayotekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ambapo jumla ya vijiji 129 vinasambaziwa umeme mkoani humo.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akiwasha umeme kwenye moja ya saluni ya mteja aliyeunganishiwa umeme katika kijiji cha Nyange wilayani Kibondo wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijiji vya wilaya za Kibondo, Kasulu na Buhigwe mkoani Kigoma hivi karibuni. Naibu Waziri Mgalu alikuwa katika ziara ya siku tatu kukagua miradi ya usambazaji wa umeme vijini inayotekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ambapo jumla ya vijiji 129 vinasambaziwa umeme mkoani humo. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Loyce Burra.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu (wapili kulia) akisikiliza maelezo toka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Loyce Burra (kuulia) mara baada ya kuwasha umeme katika Zahanati ya Kijiji cha Nyange na Saluni ya mkazi wa kijiji hicho wakati ziara yake ya kukagua miradi ya usambazaji wa umeme vijini mkoani Kigoma inayotekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ambapo jumla ya vijiji 129 vinasambaziwa umeme mkoani humo. Kushoto ni Diwani wa Viti Maalum Kata ya Mabamba,Mektrida Ngugwa.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akisikiliza maelezo ya Mkandarasi wa Usambazaji Umeme katika vijiji vya Wilaya za Kasulu, Buhigwe na Uvinza Kampuni ya CCCE – ETERN wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme katika vijiji vilivyopo katika Mpango wa Usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Tatu mzunguko wa kwanza (REA III) mkoani Kigoma hivi karibuni.
Kaimu Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa, Mtabira 825 KJ kilichopo wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Meja Peter Lyanga akizungumza walipotembelewa na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu kwa lengo la kujionea maendeleo ya usambazaji umeme katika Kikosi hicho hivi karibuni. Naibu Waziri Mgalu alikuwa katika ziara ya siku tatu kukagua miradi ya usambazaji wa umeme vijini inayotekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ambapo jumla ya vijiji 129 vinasambaziwa umeme mkoani humo. Kibondo vijiji 40, Kakonko vijiji 29, Buhigwe 21, Kasulu 12 Uvinza 10 na Kigoma vijijini 17.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akizungumza na vijana wa program ya hiari wa Jeshi la Kujenga Taifa alipotembelea Kambi ya Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa, Mtabira 825 KJ kilichopo Kasulu mkoani Kigoma kwa lengo la kujionea maendeleo ya usambazaji umeme katika Kikosi hicho hivi karibuni. Naibu Waziri Mgalu alikuwa katika ziara ya siku tatu kukagua miradi ya usambazaji wa umeme vijini inayotekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ambapo jumla ya vijiji 129 vinasambaziwa umeme mkoani humo.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Shunga na Lugoma wilayani Kasulu wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya usambazaji umeme vijijini mkoani Kigoma hivi karibuni. Naibu Waziri Mgalu alikuwa katika ziara ya siku tatu kukagua miradi ya usambazaji wa umeme vijini inayotekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ambapo jumla ya vijiji 129 vinasambaziwa umeme mkoani humo.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akifurahia jambo mara baada ya kuzindua zoezi la kuwasha umeme katika baadhi ya nyumba za wananchi wa mtaa wa Ruhita wilayani Kasulu wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya mradi wa usambazaji umeme vijijini mkoani Kigoma hivi karibuni. Naibu Waziri Mgalu alikuwa katika ziara ya siku tatu kukagua miradi ya usambazaji wa umeme vijini inayotekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ambapo jumla ya vijiji 129 vinasambaziwa umeme mkoani humo. Wapili kutoka kulia ni Meneja Mradi wa Usambazaji Umeme Vijini Mkoa wa Kigoma toka REA. Mhandisi, Oscar Benedict Migani.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akiwasha umeme akiwasha umeme katika jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya mardi wa usambazaji umeme vijijini mkoani humo hivi karibuni. Naibu Waziri Mgalu alikuwa katika ziara ya siku tatu kukagua miradi ya usambazaji wa umeme vijini inayotekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ambapo jumla ya vijiji 129 vinasambaziwa umeme mkoani humo.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akiwasha umeme akiwasha umeme katika jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya mardi wa usambazaji umeme vijijini mkoani humo hivi karibuni. Naibu Waziri Mgalu alikuwa katika ziara ya siku tatu kukagua miradi ya usambazaji wa umeme vijini inayotekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ambapo jumla ya vijiji 129 vinasambaziwa umeme mkoani humo.
Mbunge wa Jimbo la Manyovu -Buhigwe mkoani Kigoma, Mhe. Albert Obama akimshukuru Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu (katikati) kwa niaba ya Serikali kutokana na hatua za kusambaza umeme katika vijiji vya wilaya ya Buhigwe wakati wa ziara ya kukagua miradi ya usambazaji wa umeme vijini inayotekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ambapo jumla ya vijiji 129 vinasambaziwa umeme mkoani humo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Kanali Michael Ngayauma.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akimkabidhi kifaa maalum cha kuunganishia umeme kwenye nyumba ambazo hazijawekewa mfumo wa kusambazia umeme kijulikanacho kama Umeme Tayari (UMETA), mkazi wa Kijiji cha Nyankoroko wilayani Buhigwe, Bibi. Melenia Kutegwa wakati wa mkutano wa hadhara katika kijiji hicho hivi karibuni. Naibu Waziri Mgalu alikuwa katika ziara ya siku tatu kukagua miradi ya usambazaji wa umeme vijini inayotekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ambapo jumla ya vijiji 129 vinasambaziwa umeme mkoani humo. Kifaa hicho kinatolewa bure kwa watu wenye ulemavu na wazee wasiojiweza, wajane ili waweze kumudu gharama za kuunganisha umeme katika makazi yao.
Sehemu ya mtandao wa usambazaji nyaya za umeme kama zinavyoonekana katika Mtaa wa Ruhita uliopo katika Halmashauri ya Mji wa kasulu mkoani Kigoma.
Moja ya nyumba ya mkazi wa Mtaa wa Ruhita, Kasulu mkoani Kigoma ikiwa imeunganishiwa umeme kupitia Mradi wa Usambazaji Umeme Vijini Awamu ya Tatu (REA III) mzunguko wa kwanza ambapo jumla ya vijiji 129 vinaunganishiwa umeme kupitia mpango huo. (Na: Mpiga Picha Wetu
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com