Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia) akikiri kuupokea Mwenge wa Uhuru wa mwaka 2019 baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Mstaafu Nicodemus Mwangela (Kushoto).
Mwenge wa Uhuru wa Mwaka 2019 utakaokimbizwa katika wilaya tatu na
Halmashauri Nne za Mkoa wa Rukwa unategemewa kuweka Mawe ya Msingi, kukagua na
kuzindua miradi 35 ya maendeleo pamoja na vikundi 11 vya wanawake, vijana na
watu wenye ulemavu ambapo miradi hiyo ina thamani ya Shilingi Bilioni
45,404,104,489.59.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo baada ya
kukabidhiwa mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia. Jenerali.
Mstaafu Nicodemus Mwangela mara tu baada ya kuvuka daraja la mto Momba mbao
ndio mpaka wa Mkoa wa Rukwa na Songwe katika Kijiji cha Kilyamatundu, Wilayani
Sumbawanga.
Mkuu wa Mkoa amesema kuwa Mwenge wa uhuru ukiwa katika Mkoa wa Rukwa
utakimbizwa umbali wa jumla ya Kilomita 832.5 kuanzia tarehe 7 hadi 11, April,
2019 nahatimae kuwakabisdi majirani Mkoa wa Katavi, ambao utakuwa mkoa wa tatu
tangu kuwashwa kwake katika mkoa wa Songwe mapema mwezi huu.
Wakati akifafanua michanganuo ya uchangiaji wa miradi hiyo Mh.
Wangangabo alisema “Wananchi Shilingi 244,524,500.00 sawa na asilimia 0.5 ya
gharama zote.Halmashauri Shilingi 619,611,106.00 sawa na asilimia 1.4, Serikali
Kuu Shilingi 16,426,480,402.00 sawa na asilimia 36.2, Wadau wa maendeleo
Shilingi 759,489,800 sawa na asilimia 1.7 Aidha, kuna mradi wa uchimbaji
makaa ya mawe ambao unathamani ya Shilingi 27,353,998,681.59 mradi huu
utakaguliwa, ambao una wastani wa asilimia 60.2 ya gharama zote.”
Kwa upande wake Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019 aliupongeza
uongozi wa mkoa wa Rukwa kwa mapokezi mazuri aliyoyapata na kuwaahidi
kutowaangusha wananchi katika ukaguzi wake wa miradi ambayo Mwenge wa Uhuru
utaipitia.
Kauli mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 ni “Maji ni haki ya kila Mtu, tutunze vyanzo vyake na tukumbuke kushiriki
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa”
0 comments:
Post a Comment