
Baadhi ya wataalamu wa maabara
wakifuatilia mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia
wakati wa mafunzo hayo yaliyowahusisha wataalamu hao kutoka sekta ya
Afya ya Binadamu na Wanyama, Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.

Mratibu wa Afya Moja Kitaifa,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka, akieleza umuhimu wa mafunzo ya
Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia kwa wataalamu wa maabara
wakatia akifungua mafunzo hayo yaliyowahusisha wataalamu hao kutoka
sekta ya Afya ya Binadamu na Wanyama, Jijini Arusha, tarehe 29 Julai,
2019.

Mwezeshaji kutoka Wizara ya
Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto akiendelea kutoa
mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia kwa wataalamu
wa maabara wakati wa mafunzo hayo, Jijini Arusha, tarehe 29 Julai,
2019.

Mshiriki wa mafunzo ya Usimamizi
wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia kwa wataalamu wa maabara, Basilius
Kilowoko, akichangia wakati wa mafunzo hayo, Jijini Arusha, tarehe 29
Julai, 2019.

Mshiriki wa mafunzo ya Usimamizi
wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia kwa wataalamu wa maabara, Fredy
Makoga, akichangia wakati wa mafunzo hayo, Jijini Arusha, tarehe 29
Julai, 2019.

Mwezeshaji kutoka Wizara ya
Afya,Zanzibar, Rukia Shani akiendelea kutoa mafunzo ya Usimamizi wa
vimelea hatarishi vya kibaiolojia kwa wataalamu wa maabara wakati wa
mafunzo hayo, yaliyowahusisha wataalamu hao kutoka sekta ya Afya ya
Binadamu na Wanyama, Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.

Washiriki wa mafunzo ya
Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia kwa wataalamu wa
maabara, wakiwa katika picha ya pamoja na Mratibu wa Afya Moja Kitaifa,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka (katikati walio kaa) mafunzo
hayo yaliyowahusisha wataalamu hao kutoka sekta ya Afya ya Binadamu na
Wanyama, Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.
*************
Na. OWM, ARUSHA
Wataalam wa maabara nchini kwa
kutumia Dhana ya Afya moja ambao ni wataalam wa maabara kutoka sekta ya
Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira
wameendelea kupewa mafunzo ya Msingi ya Usimamizi na udhibiti wa
vimelea hatarishi vya kibailojia kwa kuimarisha ulinzi na usalama wa
sampuli za vimelea hivyo.
Vimelea hatarishi vya kibailojia
vinaweza sambaza magonjwa kwa wanyama na binadamu iwapo ulinzi na
usalama wake hautaimarishwa wakati wa kuvichukua kwa wanyama, binadamu
na mimea au wakati wa kusafirisha vimelea hivyo na kuvipeleka maabara
kwa ajili ya Uchunguzi pia wakati kuvifanyia uchunguzi pamoja na
wakati wa kuviharibu mara baada ya kuvifanyia uchunguzi.
Akiongea wakati wa kufungua
mafunzo hayo, leo tarehe 29, Julai, 2019, Mratibu wa Afya Moja Kitaifa,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka amefafanua kuwa Mafunzo hayo ni
mwendelezo wa mafunzo ya msingi ambayo wataalam hao tayari
walishafundishwa mafunzo ya awali ya Usimamizi na Usalama wa vimelea
hatarishi vya kibailojia mnamo mwezi Machi, mwaka huu.
“Lengo la mafunzo haya ni
kuiwezesha nchi yetu kuwa na wataalamu wa maabara wenye uelewa kuhusu
dhana za vihatarishi vya kibaiolojia, ikiwemo wakati wa kusafirisha
vimelea hivyo na kuvipeleka maabara kwa ajili ya Uchunguzi pia wakati
kuvifanyia uchunguzi pamoja na wakati wa kuviharibu mara baada ya
kuvifanyia uchunguzi” amesema Chinyuka
Wakiongea kwa nyakati tofauti
washiriki wa mafunzo hayo wamebainisha kuwa baada ya mfunzo hayo,
mienendo na matendo yao wakiwa maabara itazingatia usalama wa afya zao
na usalama wa jamii inayowazunguka pamoja na Usalama wa watanzania, kwa
kusimamia na kudhibiti vihatarishi vya kiulinzi na usalama vitokanavyo
na vimelea hatarishi amabavyo wataalamu hao wamepewa dhamana ya
kuvifanyia kazi.
Mafunzo hayo ya siku tano,
yameandaliwa na DTRA na Sandia National Laboratories na wawezeshaji wa
hapa nchini kutoka wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii,Jinsia , Wazee na
watoto pamoja na Wizara ya Uvuvi na Mifugo, chini ya Uratibu wa Ofisi ya
Waziri Mkuu.
Afya Moja ni dhana ni dhana
inayojumuisha sekta ya afya ya binadamu , wanyamapori, mifugo na
mazingira katika kujiandaa , kufuatilia na kukabili magonjwa
yanayoathiri binadamu ,wanyamapori na mifugo.
0 comments:
Post a Comment