Wadau walioshiriki Kikao cha Kupitisha
Mpango Kazi wa Taifa wa Kupunguza matumizi ya Zebaki kwa wachimbaji
wadogo jijini Dodoma leo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
……………….
Tanzania yadhamiria kupunguza matumizi ya Zabaki kwa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kwa asilimia 30% ifikapo 2024.
Katika kikao cha kupitisha Mpango Kazi wa
Taifa wa kupunguza matumizi ya Zebaki kwa wachimbaji wadogo
kilichoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais na kushirikisha sekta husika,
leo katika Chuo cha Biashara (CBE) jijini Dodoma, Ikiwa sehemu ya
Maandalizi ya utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa wa Minamata ambao
Tanzania ipo kwenye mchakato wa kuridhia.
Zebaki imetajwa kuwa moja kati ya
kemikali kumi hatarishi zilizo orodheshwa na Shirika la Afya Duniani na
ina madhara makubwa haswa kwenye magonjwa ya mfumo wa fahamu.
Tanzania inakadiriwa kuwa na wachimbaji
wadogo milioni 1.2, asilimia 20-30 ni wachimbaji wanawake ambapo sehemu
kubwa ya wachimbaji hawa hutumia zebaki huku kukiwa na makisio ya mwaka
ambapo tani 13 mpaka 24 hutumika na huingizwa nchini kinyemela.
Zaidi ya 25-33% ya wachimbaji wadogo
wadogo wameathirika na matumizi ya zebaki,hivyo Serikali imedhamiria
kupunguza ama kuondosha matumizi ya zebaki kwa wachimbaji wadogo.
Wakizungumza mara baada ya kumaliza kikao
hicho Bi. Noela R. Magoche ambaye ni mdau wa Madini alisema kuwa
zifikiriwe mbinu mbadala kunusuru watoto wanaofanya kazi migodini kwani
ndio waathirika wakubwa wa zebaki huku akisisitiza sheria
inayokataza ajira kwa watoto
Kwa upande wake mdau wa Mazingira Bw. Haji Rehani amesema zebaki imetambulika kimataifa kwa madhara makubwa ya kiafya.
0 comments:
Post a Comment