Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania imeweka sheria, taratibu na miongozo ambayo inashirikiana na
mashirika yasiyo ya kiserikali kuhakikisha usalama na ustawi wa watoto
nchini Tanzania.
Hata hivyo, pamoja na yote hayo bado
ukatili dhidi ya watoto umeendelea kushamiri pamoja na wahusika
kuchukuliwa hatua za kisheria. Hii inatupa picha kwamba bado
kunahitajika mkakati madhubuti wa kuhakikisha sheria zinazowekwa
zinapunguza masuala ya ukatili kwa watoto kama sio kwisha kabisa.
Serikali na wadau wanaitakia nchi yetu
mafanikio wafungue macho dhidi ya ukatili huu kwani watoto wengi
wanakutwa na majanga ya kubakwa na kulawitiwa wawapo njiani
wanapoelekea shuleni , wanapocheza na wenzao au wanapoelekea dukani
kufata mahitaji wanayoagizwa na wazazi wao
Kwa bahati mbaya sana wahusika wengi
wanaowafanyia watoto ukatili ni sehemu ya familia ya watoto husika. Mara
nyingi unakuta ni aidha, wazazi, baba wadogo , wajomba, mama wa kambo,
jirani, rafiki wa familia na jamii ya karibu na anapoishi mtoto.
Baba wa kambo mkazi wa buguruni amlawiti
mtoto wa umri wa miaka 4 , Baada ya kuachiwa na mkewe amuamshe iliaweze
kumuandaa kwenda shule na muhusika alikamatwa baaada ya mtoto kusema
kitendo anachofanyiwa na baba huyo, baadae muhusika alipewa dhamana na
kutoka kwa dhamana.
Aidha kutokana na jamii kutokuwa na
ufahamu wa kutosha kuhusu sheria na taratibu za kufuata mara baada ya
mtoto kufanyiwa ukatili wa aina yeyote ile. Suala la utamaduni au
desturi na mila ya kuamua kumaliza kimyakimya masuala hayo ya ukatili
kwa kisingizio cha kulinda heshima ya mkosaji na kumlindia hadhi katika
jamii ndio chanzo cha kuongezeka kwa masuala hayo.
Changamoto hizi zinawafanya wazazi
kushindwa kuwatoa watoto wao kwenye mambo tofauti ya kijamii kutokana
na kuogopa kutokea kwa matatizo kama hayo. Aidha kesi zikipelekwa katika
sehemu husika, wenye ushahidi kutokwenda mahakamani au mara nyingine
mhusika kutoroka na baadae kesi hufutwa bila kujua hatma ya mtoto
aliyepata madhara.
Mpaka sasa kuna idadi kubwa ya watoto
waliobakwa na kulawitiwa ambapo mwaka 2015/2016 watoto aliobakwa na
kulawitiwa walikuwa 394 na mwaka 2016/2017 kufikia 2,984 ,Tafiti
zinaonyesha idadi ya watoto waliobakwa itazidi kuongezeka kwa mwaka 2018
na 2019 na kuwa kubwa zaidi.
Suala hili sio la Serikali peke yake
ushirikiano unahitajika kutoka kwa jamii yote kwa ujumla ili kushiriki
katika kutokomeza uhalifu huu ambao unatupelekea kuwa na Taifa lisilofaa
hapo baadaye. Pia, nguvu za ziada zinahitajika kuhakikisha watoto
wanaokumbwa na majanga haya kusaidiwa kisaikolojia ili kurudi katika
hali yao ya kawaida itakayowafanya kuwa Rais wema na wazazi hapo
baadaye.
Mmoja wa wazazi wa mtoto aliye fanyiwa
ukatili wa kijinsia mkazi wa singida alisema hatutakiwi kuwa na imani
juu ya watu ambao wanatuzunguka kwani wengi wanatufanyia mambo haya ni
miongoni mwa hawa tunaoishi nao na hii hutokana na matamanio yao ya
kimwili.
Jamii kwa ujumla inatakiwa iwemacho
kupinga vikali ukatili huu unaowakumba watoto wadogo kwani wao ndio
taifa la kesho na ndio tegemeo kubwa la taifa kwa mwaka ujao hivyo
tunapofumbia macho matukio kama haya na kutokukaa kimya pale
tunapogundua kama mtoto amefanyiwa ukatili basi lazima tuchukue hatua ya
kupeleka mashtaka ya kitendo hicho mbele ya sheria .
“Tunatakiwa tufungue macho juu ya haya
matukio yanayowakuta watoto wetu na pia tuwe makini na jamii
inayotuzunguka kwa ujumla kwani wengi wao ndio wanaohusika na vitendo
hivi kwa watoto na badae kutoka hivyo serikali tunaiomba iwe macho juu
ya matukio kama haya “.
Mapendekezo yangu kama raia mwema wa
Tanzania viongozi mbalimbali wakiwemo wa dini na viongozi wa serikali
wanajitahidi kupiga vita juu ya ukatili wa namna hii kwa jamii lakini
hali bado ni tete kwani watuhumiwa wengi wa matukio haya wamekuwa
hawajui wala kuelewa juu ya vita vinavyoendelea dhidi ya ukatili kwa
watoto .
Ushauri wangu Sheria zitakazotungwa ziwe
kali kwa kuweka amani na utulivu, pia serikali ingetoa elimu juu ya
matukio ya ulawiti na hasara zake kwa jamii pia kuwajulisha juu ya
sheria zinazotumika kuwaadhibu watendaji wa matukio ya ulawiti na
ubakaji ili kuweza kupunguza utokeaji wa matukio kama haya kwa asilimia
kubwa .
Jamii ikiwa macho dhidi ya matukio haya
basi watoto wengi watakuwa salama dhidi ya matukio ya ukatili pia
kuwapeleka wahusika wa matukio haya polisi ili sheria ifate mkondo wake
basi yaweza pelekea nchi ikawa huru na amani .
0 comments:
Post a Comment