Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akizungumza jambo wakati wa kikao chake
na Balozi wa Jamhuri ya Korea Nchini, Tae-ick Cho (katikati) wakati wa
mazungumzo yao yaliyofanyika leo (Ijumaa Julai 5, 2019) katika Ofisi za
NBS Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mtaalamu wa Utafiti wa Ubalozi wa
Korea, Hae-ju Yong
Balozi wa Jamhuri ya Korea, Tae-ick Cho
akizungumza jambo wakati wa kikao chake na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya
Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa yaliyofanyika leo Ijumaa Julai
5, 2019 katika Ofisi za NBS Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja
Takwimu za Kilimo wa NBS, Titus Mwisummba na Mkurugenzi wa Takwimu za
Uchumi wa NBS, Bw. Daniel Masolwa.
Balozi wa Jamhuri ya Korea, Tae-ick Cho
akimwonesha nakala ya jarida Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu, Dkt. Albina Chuwa kuhusu miradi mbalimbali ya Maendeleo
inayotekelzwa na Serikali ya Nchi hiyo Tanzania. Kushoto ni Mkurugenzi
wa Takwimu za Uchumi wa NBS, Bw. Daniel Masolwa. Mkutamo baina ya Balozi
huyo na NBS ulifanyika leo Ijumaa (Julai 5, 2019) katika Ofisi za NBS
Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Jamhuri ya Korea, Tae-ick Cho
(kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa (katikati) na baadhi ya watendaji wa NBS
akiwemo Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi- Daniel Masolwa kulia, mara
baada ya kumalizika kwa kikao baina yao leo (Ijumaa Julai 5, 2019)
katika Ofisi za NBS Jijini Dar es Salaam.
(PICHA NA MAELEZO)
……………….
Na Mwandishi Wetu,
MAELEZO
DAR ES SALAAM
BALOZI wa Jamhuri ya Korea, Tae-ick Cho
amesema Serikali ya Nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Ofisi ya Taifa
ya Takiwmu (NBS) kwa ajili ya kuimarisha miundombinu yake ikiwemo mifumo
ya Tekonojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na kumalizia Ujenzi wa
Ofisi za NBS katika Mikoa ya Dodoma na Kigoma.
Akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa NBS,
Dkt. Albina Chuwa leo Ijumaa (Julai 5, 2019) Jijini Dar es Salaam,
Balozi Cho amesema Serikali yake ipo tayari kutoa ushirikiano
unaohitajika katika kuhakikisha kuwa NBS inatekeleza majukumu yake.
Balozi Cho alisema Serikali ya Jamhuri ya
Korea inatambua umuhimu wa takwimu katika shughuli za kuharakisha
maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika Nchi zinazoendelea ikiwemo
Tanzania, hivyo itahakikisha kuwa mahitaji yote ya msingi kwa
yanayohitajika na NBS ikiwemo uimarishaji wa miundmbinu ya TEHAMA
inapewa kipaumbele.
Mwezi Juni mwaka 2018, tulianza
mazungumzo ya ushirikiano na NBS kupitia Wizara ya Fedha na Mipango,
hivyo utekelezaji wa masuala yote ya msingi katika mazungumzo hayo yapo
katika hatua nzuri na nitawasiliana na Serikali yetu ili kuona jinsi ya
kusukuma jambo hili kwa haraka zaidi.
Aidha Balozi Cho aliongeza kuwa Serikali
ya Korea itahakikisha kuwa makubaliano hayo yanaanza kutekelezwa kwa
haraka kwa kuwa inatambua ukubwa na umuhimu wa majukumu ya NBS katika
uzalishaji na upatikanaji wa takwimu kwa ajili ya kuharakisha shughuli
za Maendeleo ya wananchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NBS,
Dkt. Albina Chuwa alisema NBS kupitia Wizara ya Fedha na Mipango tayari
ilianza hatua za awali za makubaliano ya ushirikiano na Serikali ya
Jamhuri ya Korea na hivyo kupitia sheria ya misaada ambapo wameahidi
kujenga na kuimarisha miundombinu ya Ofisi za NBS zilizopo katika Mikoa
ya Kigoma na Dodoma.
“Katika Mkoa wa Kigoma wameahidi kujenga
Ofisi hiyo na kusimika miundombinu ya TEHAMA wakati katika Mkoa wa
Dodoma wameahidi kuweka miundombinu ya TEHAMA katika Jengo la Ofisi zetu
za Dodoma” alisema Chuwa.
0 comments:
Post a Comment